26.2 C
Dar es Salaam
Monday, October 3, 2022

MJI WA MOSCOW WATIKISA KWA VIVUTIO KOMBE LA DUNIA

BADI MCHOMOLO NA MITANDOA


KUANZIA Juni 14, wadau na mashabiki wa soka duniani watatumia muda wa mwenzi mmoja kuangalia nini kinaendelea nchini Urusi kutokana na michuano ya Kombe la Dunia kufanyika huko.

Huku watu wakifuatilia kupitia vyanzo mbalimbali vya habari, lakini wale ambao watabahatika kwenda nchini humo kuangalia kivumbi hicho wanaweza kupata fursa ya kutembelea vivutio mbalimbali ambayo vinatikisha nchi hiyo.

Moscow ni mji mkuu wa nchini Urusi, unatajwa kuwa miongoni mwa miji ambayo ina vivutio mbalimbali vya watalii, hivyo SPOTIKIKI leo hii imekutajia baadhi ya vivutio vinavyotikisa kwenye mji huo.

Red Square

Ni moja ya makanisa mjini Moscow mbalo limekuwa kivutio kwa kiasi kikubwa katika nchini nzima ya Urusi. Kanisa hilo linajulikana kwa jina la Red Square, sasa limekuwa kama sehemu ya kivutio kwa watalii.

Inasemekana kuwa kanisa hilo lilijengwa karne ya 16, hata hivyo mjenzi wa kanisa hilo ambaye alikuwa anajulikana kwa jina la Ivan, alikamatwa mara baada ya kumaliza ujenzi kwa madai kwamba kwa nini alijenga kanisa zuri kama hilo.

Kanisa La Cathedral

Linatajwa kuwa ni kanisa la kwanza kwa ukubwa duniani, lipo karibu kanisa la Red Square lililojengwa karne ya 16. Kanisa hilo la Cathedral lina urefu wa mita 103, ambazo ni sawa na futi 338.

Hata hivyo kanisa hilo lilikuwa linatumika na waandamanaji wa Pussy Riot, ambao walikuwa wanampinga rais wa nchi hiyo Vladimir Putin mwaka 2012.

Zaryadye Park

Hii ni sehemu mpya ya mji wa Moscow, ambayo imegawanywa mara nne kwa ajili ya watalii wa aina mbalimbali, kuna sehemu kwa ajili ya mafuriko ya maji, sehemu nyingine ni kwa ajili ya mbuga za wanyama.

Kitu kingine kikubwa cha kivutio ni daraja inayozunguka katika eneo mbalimbali ya hifadhi pamoja na sehemu mbalimbali za mafuriko ya maji.

Bolshoi theatre

Ni moja kati ya majengo ya maonyesho ambayo yanatajwa kuwa ni makubwa duniani, ndani ya jengo hilo kuna michezo mbalimbali hivyo watalii ujitokeza kwa wingi hata kama sio wapenzi wa michezo, lakini ni historia kuingia kwenye jengo hilo.

Gorky Park

Hilo ni moja kati ya majengo yenye kuvutia watalii kwa ajili ya kushuhudia mambo mbalimbali ya tamaduni za nchi ya Urusi.

Mbali na kuona mambo ya kitamaduni, lakini kuna sehemu za kupata burudani mbalimbali za muziki, kuangalia filamu, ngumi pamoja na sehemu ya kupumzika familia.

  1. Moscow metro (Usafiri Wa Chini)

Huu ni usafiri ambao unapendwa na watalii wengi nchini Urusi katika mji wa Moscow na unatajwa kuwa wa haraka kuliko usafiri mwingine wa barabarani kwa kuwa hakuna foleni yotote kutoka sehemu moja kwenye nyingine.

Usafiri huo unatumia treni, hata hivyo treni hizo zinapita chini kwa chini kutokana na aina ya mihundo mbinu iliotengenezwa ya kupita chini ya ardhi.

Usafiri huo unatumika kwa ajili ya kwenda kwenye vituo mbalimbali kama vile Mayakovskaya, Ploshad Revolutsii, Kievskaya, Kropotkinskaya, Kurskaya, Komsomolskaya na Novoslobodskaya.

Waenda Kwa Miguu (Arbat streets)

Mjini Moscow kuna sehemu ambayo inajulikana kwa jina la Arbat Street, hii ni mitaa ambayo inatumika kwa watu waenda kwa miguu, hakuna usafiri wowote ambao unatumika kutokana na sheria zilizowekwa.

Arbat Street ni mtaa wenye umbali wa kilometa moja, hivyo watu wanakutana kila kona kwa ajili ya kutembea kwa miguu, hakuna baiskeli, pikipiki, gari wala kifaa chochote kwa ajili ya safari.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,573FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles