26.2 C
Dar es Salaam
Monday, October 3, 2022

TIMU ZA TAIFA ZITAFIKIA KWENYE HOTELI HIZI URUSI (2)

BADI MCHOMOLO NA MITANDAO


TIMU 32 za Taifa zinatarajia kuweka kambi nchini Urusi kwa ajili ya michuano ya Kombe la Dunia, hiyo ni nafasi moja wapo ya nchi ya Urusi kuongeza pato la taifa na kukuza kwa uchumi wao.

Tukio hilo la Kombe la Dunia litakuwa la mwezi mmoja, lakini zipo timu ambazo zitaondolewa mapema kwenye michuano hiyo na hatimaye kurudi nyumbani, leo hii SPOTIKIKI ipo sehemu ya pili kukuelezea hoteli zingine nane ambazo zimechaguliwa kwa ajili ya timu kuweka kambi zao.

Croatia

Katika mji wa Saint Petersburg, timu ya taifa ya Croatia ameamua kuchagua kuwa sehemu yao ya kuweka kambi kwa ajili ya michuano hiyo ya Kombe la Dunia, hivyo imeitaja hoteli ya Woodland Rhapsody resort complex kuwa ndio kambi yao.

Hoteli hiyo ipo mbali umbali wa kilomita 60, pembezoni kidogo ya mji wa St. Petersburg. Hoteli hiyo haina ukubwa sana, ila ina jumla ya vyumba 74, huduma mbalimbali zinapatikana kama vile, mgahawa, lounge, ukumbi wa mkutano.

Ipo katika mazingira mazuri kwa ajili ya kupumzika kutokana na miti iliozunguka pamoja na ziwa, kuna uwanja mdogo wa michezo, swimming pool, gym pamoja na chumba cha kunyoosha mwili. Hoteli hiyo imejengwa kwa ajili ya Kombe la Dunia.

Denmark

Taifa la Denmark limeamua kwenda kuweka kambi kwenye mji wa Apana nchini Urusi na kuweka kambi kwenye hoteli ya Beton Brut kwa kipindi chote cha michuano ya Kombe la Dunia.

Mji huo wa Anapa unatajwa kuwa miongoni mwa miji ambayo ina watalii wengi kipindi cha likizo, mji huo upo Kusini Magharibi mwa mji wa Krasnodar na upo kilometa 360 kutoka Kaskazini Magharibi mwa mji wa Sochi. Mji huo wa Apana umetajwa kuwa na nyuzi joto 21-25 wakati wa majira ya joto.

Hoteli hiyo ina swimming pools mbili, eneo kubwa la mchanga wa bahari na timu hiyo ya Denmark itatumia uwanja wa klabu ya Spartak kwa ajili ya mazoezi.

 

Ufaransa

Paulo Pogba, pamoja na wachezaji wenzake wa nchini Ufaransa watafikia kwenye mji wa Moscow, katika hoteli ya Hilton Garden Inn New Riga kwa ajili ya michuano hiyo.

Hoteli hiyo ina sehemu ya huduma ya afya, ukumbi wa cinema, swimming pool, Jacuzzi, chumba cha kuweka sawa mwili, pamoja na mambo mengine mbalimbali ya kimichezo.

Timu hiyo ya taifa itafanya mazoezi kwenye uwanja wa Glebovets. Uwanja huo umekuwa ukitumika na ligi mbalimbali za mji huo pamoja na Wilaya ya Istrinsky.

 

Ujerumani

Kikosi cha timu ya taifa ya Ujerumani itaweka kambi kwenye mji wa Moscow, katika hoteli ya Vatutinki Health Complex.

Hoteli hiyo ipo Kusini magharibi mwa mji wa Moscow na ipo karibu na mto Desna, uliopo kilometa 16 kutoka kwenye mji huo.

Ndani ya hoteli hiyo kuna huduma mbalimbali kama vile Sweimming pool, Pool table, darts, tenisi, paintball na michezo mingine mbalimbali.

timu hiyo imepata uwanja wa Verdant Neighbourhood ambao unatumiwa na CSKA Moscow, uwanja huo una nyasi za hasiri na una sehemu ya kufanyia mikutano na wanahabari na vyumba vya kubadilishia nguo.

Iceland

Gelendjik ni mji ambao timu ya taifa ya Iceland imeamua kwenda kuweka kambi kwa ajili ya michuano hiyo ya Kombe la Dunia, pia imechagua hoteli ya Nadezhda Resort Complex kwa kipindi ambacho watakaa.

 

Gelendjik ni mji ambao una unyevunyevu kwa mbali, lakini mara kwa mara kuna upepo, upepo huo unakimbiza joto. Hoteli ya Nadezhda Resort Complex ipo umbali wa kilometa 250 kutoka Kaskazini Magharibi mwa mji wa Sochi.

Olimp Stadium ni uwanja ambao Iceland utautumia kwa ajili ya maandalizi ya michuano hiyo, uwanja huo unatumiwa na michuano mbalimbali ya shule.

 

Iran

Timu ya Iran inatarajia kuweka kambi kwenye hoteli ya Bakovka complex, iliopo mji wa Moscow na itatumia uwanja wa FC Lokomotiv kwa ajili ya mazoezi.

 

Bakovka complex ni hoteli ambayo unapata huduma ya Internet, Gym, swimming pool, pia ina viwanja viwili kwa ajili ya kufanyia mazoezi ya mpira wa miguu.

Japan

Mji wa Kazan ndipo ambapo timu ya Taifa ya Japan imeamua kwenda kuweka kambi kwa ajili ya Kombe la Dunia, pia itatumia uwanja wa FC Rubin training base kwa ajili ya mazoezi.

timu hiyo itaweka kambi kwenye hoteli ya The Base, hoteli hiyo ina enel lenye ukubwa wa Square Metres 4666, ndani yake kuna sehemu ya huduma ya afya, mgahawa, Gym pamoja na huduma zingine mbalimbali za michezo.

 

Korea Kusini

Timu ya taifa ya Korea Kusini, itaweka kambi kwenye hoteli ya New Peterhof, iliopo kwenye mji wa Leningrad. Hoteli hiyo ilifunguliwa tangu mwaka 2010.

 

Hoteli hiyo ina sehemu ya kupasha mwili joto, swimming pool na gym. Uwanja ambao watautumia kwa ajili ya mazoezi ni Spartak Stadium, upo kilometa chache kutoka Peterhof.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,573FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles