24.2 C
Dar es Salaam
Monday, September 27, 2021

Mitandao ya kijamii kudhibitiwa Marekani?

 WASHINGTON, MAREKANI 

RAIS wa Marekani, Donald Trump ameamua kuweka saini ya kuondoa baadhi ya marufuku ya kisheria ambayo mitandao ya kijamii inayo. 

Saini hiyo inampa mamlaka ya kuweka hatua za kisheria dhidi ya kampuni za mitandao ya kijamii kama Facebook na Twitter katika sheria walizoweka katika maudhui wanayochapisha katika mitandao yao. 

Rais Trump ameishutumu mitandao ya kijamii kwa kushindwa kuwa makini wakati wa kusaini mamlaka ambayo iko huru kuondolewa wakati wa kuweka saini. 

Amri hiyo inatarajiwa kukabiliwa na changamoto za kisheria. 

Wataalamu wa kisheria wanasema kuwa bunge la Marekani au mfumo wa mahakama lazima ihusike ili kubadili sheria iliyopo sasa ambayo inaeleweka kuwa inalinda mitandao ya kijamii. 

Donald Trump ameilaumu Twitter kwa kuingilia uchaguzi wa urais wa Marekani wa 2020

Trump amekuwa akiishutumu mitandao ya kijamii kila mara kuhariri sauti yake au hata kuweka sauti ambayo hajazungumza lakini anakuwa anasikika kama yeye. 

Jumatano, Trump aliishutumu Twitter kwa kuingilia uchaguzi baada ya kuongeza maelezo ya tweet mbili kama uthibitisho. 

 Alhamisi , Twitter iliongeza taarifa za kuhakiki taarifa kuhusu Covid-19” na kujumuisha ujumbe wa tweet kutoka kwa msemaji wa serikali ya China anayedai kuwa virusi vya corona vilitengenezwa Marekani. 

Amri hiyo inasemaje? 

Amri hiyo imewekwa ili kufafanua sheria ya mawasiliano ya staha ambayo Marekani imeweka katika mitandao ya kijamii kama Facebook, Twitter na Youtube pamoja na ulinzi wa kisheria katika hali fulani. 

Chini ya kifungu cha sheria cha namba 230, mitandao ya kijamii haiwajibishwi kwa maudhui ambayo watumiaji wake wanaweka mtandaoni lakini inaweza kuhusika kwa upande wa usamaria mwema wa kuondoa maudhui hayo mtandaoni ambayo labda yana maudhui ya unyanyasaji, chuki na yanaaibisha . 

Amri hiyo maalumu inaainisha kuwa sheria ambayo italinda maudhui ya mitandao ya kijamii kama maudhui hayo hayajabilishwa kwa kuhaririwa na mtumiaji wa mtandao huo na kutaka sheria hiyo ibadilishwe au kuondolewa na wabunge kwa kifungu namba 230. 

Trump alisema Mwanasheria Mkuu, William Barr ataanza mara moja kuandaa sheria ambayo itapigiwa kura. 

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
158,310FollowersFollow
519,000SubscribersSubscribe

Latest Articles