Minziro ataja vitu alivyoanza navyo Mbao

0
675

Na WINFRIDA MTOI- DAR ES SALAAM

KOCHA Mkuu wa Mbao, Fred Minziro, ameweka wazi maeneo aliyoanza kuyasuka ili  kuinusuru timu hiyo na  janga la kushuka daraja.

Minziro alikabidhiwa majukumu ya kuinoa Mbao wiki iliyopita akichukua nafasi ya Hemedi Suleiman ‘Morocco’, aliachana na kikosi hicho tangu mwaka jana.

Alizungumza na MTANZANIA jana kabla ya mchezo wao na Coastal Union, Minziro alisema kwa siku  alizofanya mazoezi na timu hiyo alijaribu  kuangalia zaidi maeneo manne.

Minziro alitaja maeneo hayo kuwa ni safu ya ushambuliaji, kumiliki mpira, ulinzi na kiungo.

“Ni ngumu kueleza kwa sasa kuwa timu itabaki au itashuka kwa sababu bado tuna mechi  zimebaki, lakini kikubwa nimejaribu kuanza na maeneo ya msingi amabyo yanaweza kutupa matokeo mazuri.

Ukiangalia nafasi tuliyopo, kinachotakiwa ni kushinda mechi  zilizobaki ili kujitoa chini, naamini   tunaweza kufanikiwa, nitachokata ni timu kucheza mpira,” alisema Minziro.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here