27 C
Dar es Salaam
Friday, May 27, 2022

Meja Mingange apiga hesabu kali kuinusuru Ndanda

Na WINFRIDA MTOI- DAR ES SALAAM

KOCHA Mkuu wa Ndanda FC, Meja Mstaafu wa Jeshi, Abdul Mingange, amesema akishinda mechi nne au tatu zinaweza kumtoa kwenye hatari ya kushuka daraja.

Katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, kabla ya mechi za jana, Ndanda ilikuwa nafasi ya 14  na pointi 34 baada ya kucheza mechi 30.

Akizungumza na MTANZANIA, juzi, alisema   michezo mitatu ni michache lakini ni ngumu kupata ushindi kutokana na hali ilivyo, kila mechi inakua ya ushindani.

Alisema katika mechi zao zilizobaki, kuna mechi ngumu za Simba na Yanga ambayo wanatarajia kukutana nayo Jumamosi hii kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

“Kazi bado tunayo ya kutoka huku chini, tulishinda mechi na Biashara, tukapanda kidogo lakini ukiangalia pointi ni kima timu hasijapishana, hivyo kitu pekee kinachohitajika ni ushindi,” alisema.

Aliaeleza kuwa anashukuru  hana majeruhi katika kikosi chake na  wachezaji wanazidi kuimarika viwango kutokana na mazoezi waliyofanya kwa kipindi cha maandalizi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
192,454FollowersFollow
541,000SubscribersSubscribe

Latest Articles