24 C
Dar es Salaam
Saturday, May 4, 2024

Contact us: [email protected]

MILIONI 400 KUIMARISHA MIUNDOMBINU MIGODI YA TANZANITE

Na JULIETH PETER-SIMANJIRO

NAIBU Waziri wa Nishati na Madini, Dk. Medard Kalemani, amesema Serikali

imetenga Sh milioni 400 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya eneo la

uwekezaji la EPZA la mji mdogo wa Mirerani wilayani Simanjiro, Mkoa wa Manyara.

Akizungumza na wamiliki wa migodi ya madini ya Tanzanite mjini Mirerani juzi, Dk. Kalemani alisema fedha hizo zimeshapatikana kwa ajili ya kuanza ujenzi wa miundombinu ya eneo hilo.

“Ukamilishwaji wa ujenzi wa EPZA Mirerani, utafuatiwa na uwepo wa soko la madini ya Tanzanite kwenye eneo hilo ili kila mtu atakayetaka kufanya biashara hiyo, aifuate hapo.

Lengo ni kuhakikisha EPZA ya Mirerani inakuwa kichochea cha maendeleo kwenye soko la madini hayo tofauti na sasa ambapo madini hayo yanayopatikana Tanzania, yanawafaidisha watu wa nchi zingine.

“Kupitia EPZA Mirerani, wanunuzi wa madini waliopo Arusha, wataondoka na kuelekea eneo hilo, hivyo kufanikisha Serikali kupata mapato yake na kudhibiti utoroshwaji wa madini hayo unaofanyika kwa njia za panya,” alisema Naibu Waziri huyo.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Wachimbaji Madini Mkoa wa Manyara (Marema), Sadiki Mneney, aliunga mkono hatua hiyo ya Serikali kuanzisha EPZA Mirerani kwa kile alichosema kuwa mpango huo utasaidia kuinua soko la madini hayo.

“Pamoja na hayo, tunamshukuru naibu waziri kwa kuwaagiza maofisa madini

kutoa semina kwa wachimbaji kila Ijumaa ya mwisho wa mwezi ili kuwapa uelewa mpana juu ya madini hayo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles