29.7 C
Dar es Salaam
Wednesday, August 17, 2022

Michelle Obama amtolea uvivu Donald Trump

Michelle Obama
Michelle Obama

Washington:  Marekani

MKE wa Rais wa Marekani, Michelle Obama amemtaja mgombea wa   urais wa chama cha Republican, Donald Trump kuwa ana  chuki ya kumdhinisha Hillary Clinton kuwa mgombea wa urais wa Chama cha Democrat.

Aliyasema hayo alipohutubia mkutano mkuu wa Democrat mjini Philadelphia, mkutano ambao unatarajiwa kumuidhinisha rasmi Hillary.

“Lugha ya chuki kutoka kwa  mtu ambaye ni kioo cha jamii kwenye runinga haiwakilisha roho ya kweli ya nchi hii,” alisema Michelle.

Katika hotuba yake, Michelle   alionekana  kumrushia maneno Trump bila kumtaja jina.

Alisema anataka mtu wa kumrithi urais mume wake, Barack Obama, awe mtu mwenye umakini na anayejua kazi  na huyo siyo mtu mwingine bali ni Hillary Clinton.

“Tunawaomba binti zetu kupuuza wale wanaohoji uraia au imani ya baba yao,” alisema.

  Erica Aniva wa Malawi, akiwa na mzizi ambao huusaga na kuweka  kwenye maji na kuunywa kabla ya kufanya ngono na wasichana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,903FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles