23.7 C
Dar es Salaam
Saturday, September 23, 2023

Contact us: [email protected]

Padre akichinjwa Ufaransa

Jacques Hamel

Paris:  Ufaransa

PADRE wa Kanisa la Katoliki nchini Ufarasa amechinjwa na watu wawili wenye visu wa kundi la ugaidi la ISIS.

Watuhumiwa hao walimkata koo padre huyo baada ya kuvamia kanisa moja na kuwateka watawa na waumini kabla kuuawa na polisi.

Watu wa tano akiwamo padre, watawa wawili na mashemasi wawili, walishikiliwa na wauaji hao walipovamia Kanisa la Saint-Etienne-du-Rouvray katika mji wa Normandy   saa 3.00 asubuhi.

Jacques Hamel (84),  alichinjwa wakati wa tukio hilo huko wateka wengine hali zao ni  mahututi hospitalini.

Wauaji hao walidhibitiwa na polisi maalumu katika mapambano makali kwenye jengo hilo..

Vyombo vya habari nchini humu vilisema  muuaji mmoja alikuwa amevaa nguo za Kiislamu na kikosi cha Ufaransa cha kupambana na ugaidi kimekwisha kuanza kuchunguza tukio hilo.

Inasemakana   sehemu za ibada ya yakiwamo makanisa Katoliki yamo kwenye orodha ya kushambuliwa na kundi la ISIS, kwa mujibu wa  taarifa zilizopatikana   Aprili mwaka huu.

Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis ameeleza kusikitishwa kwake  na mauaji ya ukatili  katika sehemu Takatifu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,701FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles