22.6 C
Dar es Salaam
Saturday, May 21, 2022

Mgombea ubunge Bariadi aanza na kero ya tembo kuvamia mashamba

Derick Milton, Simiyu

Mgombea ubunge Jimbo la Bariadi Mkoani Simiyu, Mhandisi Andrew Kundo (CCM), amezindua kampeini za kusaka nafasi hiyo, huku akitangaza kuhakikisha anawatumikia wananchi kwa juhudi na kasi kubwa.

Katika uzinduzi huo, mgeni rasmi alikuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashuari Kuu ya chama hicho, Kassim Majaliwa, ambapo kundo aliomba kutatuliwa kwa changamoto ya uvamizi wa tembo katika mashamba na makazi ya watu.

Mgombea huyo amesema kuwa changamoto hiyo imekuwa ya muda mrefu, kwa wananchi wa vijiji ambavyo vinapakana na hifadhi ya pori la akiba la Maswa licha ya kuzalisha kwa wingi lakini tembo wamekuwa wasumbufu.

Amesema kuwa wanyama hao wamekuwa wakivamia mashamba yao pamoja na nyumba na kusababisha uharibifu, ambapo amemuomba Waziri mkuu kuwasaidia kuwapatia gari la kupambana na wanyama hao.

“Sisi wanabariadi ni wakulima wa zao la pamba kama zao la biashara na mazao ya chakula, lakini tuna changamoto kidogo sana kwenye kata za Mwasinasi, Ihusi, Halawa, Gibeshi na Matongo tuna tatizo la tembo kuvamia, wananchi hawa wamekuwa wakishinda mashambani kulinda wanyama hawa, tunaomba hata kwa kuanzia tupewe gari la doria ambalo litasaidia kupambana na changamoto hii ,” amesema Kundo.

Aidha Mgombea huyo aliomba kutengenezwa kwa Barabara ya Nkololo hadi Bariadi, kutokea mgodi wa Bulumbaka Gasuma ili iweze kupitika mara kwa mara kutokana na umuhimu wake kwa wananchi.

Akimnadi mgombea huyo, Waziri Mkuu amesema kuwa Chama hicho kilimteua Kundo kutokana na uchapakazi wake na kumuanini kuwa atawaletea maendeleo makubwa wananchi wake.

Majaliwa amesema kuwa wananchi wanatakiwa kumpigia kura pamoja na madiwani wa CCM ili kuweza kuendelea kuletea maendeleo hasa kuboresha huduma za Afya, Elimu pamoja na maji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
191,647FollowersFollow
541,000SubscribersSubscribe

Latest Articles