25.3 C
Dar es Salaam
Monday, July 4, 2022

Mosha: Nifuteni machozi kwa kumpa kura Tarimo Moshi Mjini

Safina Sarwatt, Moshi

Aliyekuwa mgombea ubunge Jimbo la Moshi Mjini (CCM), Devis Mosha na kuangushwa na mgombea wa Chadema, Jafary Michael amewaomba wakazi wa Moshi kumfuta machozi kwa kumchagua mgombea wa CCM, Prisscus Tarimo katika Uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu.

Mosha amesema endapo wananchi wa Moshi watamchagua Tarimo atahakikisha ahadi zake alizozitoa mwaka 2015 wakati akigombea ubunge jimbo hilo anazitekeleza ikiwemo kuishinikiza serikali kufufua viwanda vilivyokufa ili kutoa ajira, kukuza uchumi wananchi wapate maendeleo.

Mosha ameyasema hayo katika mkutano wa kampeni akimuombea kura mgombea urais Dk. John Magufuli na mgombea ubunge katika mkutano wa hadhara uliofanyikia katika mtaa wa kalimani kata ya kaloleni.

Mosha amesema mwaka 2015 aligombea ubunge kwa  nia ya kuwaletea maendeleo wananchi wa Moshi  lakini kura zake hazikutosha baada ya mpinzani wake kumuangusha na sasa hana chuki wala kinyongo chochote kwani nia yake ilikuwa ni kulikomboa jimbo la Moshi lilochukuliwa na upinzani kwa miaka 25 sasa ili kuleta maendeleo ya wananchi wa moshi.

Mosha amesema kwa sasa amekomaa kisiasa na wakazi wa manispaa ya Moshi wanakabiliwa na changamoto nyingi na kwamba wakitaka kumfuta machozi wampe kura za kutosha Priscus Tarimo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
195,649FollowersFollow
545,000SubscribersSubscribe

Latest Articles