26.1 C
Dar es Salaam
Friday, December 9, 2022

Contact us: [email protected]

Mbeya City anga moja na Juventus, Leicester City

Klabu ya Mbeya City, Juventus pamoja na Leicester City zimeingia kwenye udhamini mpya na kampuni ya michezo ya kubahatisha ya Parimatch www.parimatch.co.tz inayoendesha shughuli zake nchini baada ya pazia la Ligi kuu soka Tanzania Bara msimu wa 2020-21 (VPL), Ligi kuu ya Uingereza (EPL) na ile ya Italia maarufu kama Seria A kufunguliwa siku za hivi karibuni.

Mwandishi wetu

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti wa Parimatch Tanzania, Tumaini Maligana ambaye amesema kwamba wamejipanga vilivyo katika kukuza na kuleta changamoto mpya kwenye soka la Tanzania kwa kuangalia katika kushirikisha vilabu vya ndani na nje ya nchi.

“Tunafuraha kubwa kutangaza kuwa washirika na Leicester City pamoja na Juventus, uhusiano huu utakuwa muhimu kwa pande zote kwa namna moja ama nyingine.

“Kiukweli ilikuwa ni ndoto yetu ya kipindi kirefu kuingia katika udhamini na klabu kubwa za kimataifa na sasa hilo tumelifanikisha na tumekuwa wa kwanza kuweka historia kwa Tanzania kufanya hivyo.

“Mbali na hayo, ni dhahiri tunaenda kuiona Mbeya City katika ‘level’ zingine ndani ya msimu huu licha ya kwamba, imeonekana kuanza kwa kususua katika mechi zake mbili za ufunguzi alizocheza ugenini kati ya KMC na Yanga SC,” amesema Maligana.

Ameongeza kuwa kila kitu ni muda na huenda mchezo unaofuata wa Septemba 20 mwaka huu dhidi ya Azam FC akavunja historia yake ya kufungwa na matajiri hao na kuanza kasi ya kutafuta ubingwa wa msimu huu na kwamba hakuna kinachoshindikana katika soka kila kitu ni jitihada na mbinu kali za kupambana na mpinzani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,734FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles