28.5 C
Dar es Salaam
Wednesday, August 17, 2022

Mgombea CUF atamba kuwa msomi kama Lipumba

Nora Damian, Dar es Salaam

Mgombea uenyekiti wa Taifa katika Chama cha Wananchi (CUF) upande wa Profesa Ibrahim Lipumba, Diana Simba, amesema si kwamba Lipumba ndiye msomi pekee  kwani hata yeye ana Stashahada ya Maendeleo ya Jamii hivyo anaamini anaweza kukiongoza chama hicho.

Diana ambaye ni mwanamke pekee anayegombea nafasi hiyo amejikuta katika wakati mgumu wakati wa kujinadi na kuomba kura kutokana na aina ya maswali aliyokuwa akiulizwa.

Elimu, uzoefu ndani ya chama na nchi alizowahi kutembelea ni kati ya maswali yaliyoelekezwa kwa mgombea huyo na alipokuwa akijibu baadhi ya wajumbe walisikika wakimkejeli hatua iliyosababisha msimamizi kuchukua kipaza sauti mara kwa mara kuwasihi watulie wamsikilize mgombea.

“Nilijiunga na chama mwaka 2017 na nimetembelea Kenya na Uganda, msifikiri Profesa Lipumba ndiye msomi peke yake hata mimi ni msomi. Nina Diploma ya Maendeleo ya Jamii hivyo nina uwezo wa kuwaongoza,” amesema Diana.

Mbali ya Lipumba wagombea wengine wa nafasi ya Mwenyekiti Taifa ni Lipumba na Zuberi Hamisi.

Hivi sasa uchaguzi huo unaendelea kwa wagombea wa nafasi za makamu mwenyekiti Zanzibar na Bara kuomba kura.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,908FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles