27 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Kura feki zaokotwa kwenye uchaguzi CUF

Na Nora Damian

Wakati uchaguzi ukiendelea katika mkutano mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) upande wa Profesa Ibrahim Lipumba, vimeokotwa vipeperushi ndani ya ukumbi vyenye majina ya watu wanaodaiwa kuwa ndio wanaopaswa kuchaguliwa.

Zoezi la uchaguzi linaendelea katika ukumbi wa Lekam Buguruni na tayari wajumbe wamepiga kura kumchagua mwenyekiti na makamu mwenyekiti kwa upande wa Zanzibar.

Mmoja wa viongozi wa Kamati ya Uchaguzi aliwaonyesha wajumbe mojawapo ya kipeperushi kilichookotwa na kusema kuwa ni feki hivyo kipuuzwe.

“Kamati ya Uchaguzi haijaandaa kitu kama hiki, ieleweke vipeperushi hivi ni feki na hatuhusiki navyo kama kamati,” amesema kiongozi huyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles