MGANGA WA KIENYEJI ATUHUMIWA KUBAKA

0
1153

NA MANENO SELANYIKA-DAR ES SALAAM


 

MGANGAMGANGA wa kienyeji, mkazi wa Kijiji cha Kirungu mkoani Kigoma, Wilson Ndaliheremo (30), amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni akikabiliwa na tuhuma za kumbaka binti (jina tunalo) mwenye umri wa miaka 19.

Mbele ya Hakimu Joyce Mushi, Wakili wa Serikali, Daisy Makakala, alidai kwamba mtuhumiwa alitenda kosa hilo Desemba 29, mwaka jana maeneo ya Kawe Ukwamani.

Katika maelezo ya hati ya mashtaka, wakili huyo alidai mtuhumiwa alimwingilia msichana huyo bila ridhaa yake kisha kumsababishia maumivu makali sehemu zake za siri.

Baada ya maelezo hayo, mtuhumiwa alikana kutenda kosa hilo.

Wakili alidai upelelezi wa shauri hilo unaendelea hivyo akaomba tarehe nyingine ya kutajwa.

Hata hivyo, Hakimu Mushi alisema kwa mujibu wa sheria shtaka hilo linadhaminika, hivyo alimtaka mtuhumiwa kuwa na wadhamini wawili walioajiriwa serikalini au katika taasisi inayotambulika kisheria, pia watakaoweka saini ya maandishi ya Sh milioni tano kila mmoja.

Mahakama imeahirisha kesi hiyo hadi Januari 30, mwaka huu itakapotajwa tena na mtuhumiwa alirejeshwa mahabusu kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here