30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, November 30, 2023

Contact us: [email protected]

JKCI YAZIBUA MOYO KWA KUTUMIA MSHIPA WA MGUU

NA VERONICA ROMWALD – DAR ES SALAAM


Bashiri NyangassaTAASISI ya Tiba ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) imefanya upasuaji wa kuvuna mishipa ya damu mguuni na kuipandikiza katika mishipa ya moyo iliyokuwa imeziba.

Upasuaji huo unaojulikana kwa kitaalamu kama Coronary Artery Bypass Graft (CABG), umefanywa na madaktari bingwa wa moyo wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao wa Hospitali ya Apollo, Bangalore ya nchini India.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji, daktari bingwa wa magonjwa ya moyo, Bashiri Nyangassa, alisema jumla ya wagonjwa sita wamefanyiwa upasuaji huo kuanzia Januari 12 hadi 16, mwaka huu.

“Kati ya wagonjwa hao, wanaume walikuwa wanne na wanawake ni wawili. Upasuaji huu ni mara ya kwanza kufanyika nchini, kama tungewapa rufaa kwenda nje Serikali ingetumia takriban Sh milioni 174 za matibabu,” alisema.

Alisema upasuaji huo uliweza kufanyika bila ya kutumia mashine ya mapafu ya moyo.

“Upasuaji mwingine uliofanyika ni wa kubadilisha milango ya moyo ambayo haikuwa inapitisha damu vizuri. Tumemfanyia mgonjwa upasuaji wa milango miwili ya moyo ambayo iliharibika sana, milango hiyo tuliibadilisha na kuipanua kwa kishina cha mshipa mkubwa wa moyo kwa kutumia mfuko wa moyo (Aorta),” alisema.

Dk. Nyanyasa alisema JKCI mwaka huu imepanga kufanya kambi mbalimbali za matibabu na kwamba watakwenda kufanya upimaji hadi shuleni.

“Tutaenda shuleni kwa sababu tumegundua watoto wengi wanasumbuliwa na maradhi haya, tunatarajia kuwa na kambi ya madaktari Afrika kuanzia Januari 23 hadi 29, mwaka huu,” alisema.

Alisema katika kambi hiyo wanatarajia kuwafanyia upasuaji wa moyo bila kufungua kifua (catheterition procedure) wagonjwa 15.

“Februari 4, mwaka huu tutakuwa na kambi nyingine tena ya madaktari bingwa kutoka Saudi Arabia. Upasuaji utafanyika bila kufungua kifua pia, tutafanya kazi ya kutanua mishipa ya moyo iliyoziba, kutanua milango ya moyo iliyoziba na kuziba matundu ya moyo,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
579,000SubscribersSubscribe

Latest Articles