22.2 C
Dar es Salaam
Friday, October 11, 2024

Contact us: [email protected]

Mfanyabiashara kizimbani akidaiwa kumpa rushwa mwanasheria CCM

KULWA MZEE-DAR ES SALAAM

MFANYABIASHARA Chandulal Walji Ladwa (68), amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala kwa tuhuma za kumpa rushwa Mkuu wa Kitengo cha Sheria wa CCM, Goodluck Mwangomango.

Ladwa alipanda kizimbani mwishoni mwa wiki na kusomewa shtaka moja na Wakili kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Veronica Chimwanda mbele ya Hakimu Mkazi Samweli Obas.

Wakili Chimwanda alidai mshtakiwa ambaye ni mfanyabiashara, mkazi wa Sea View, mtaa wa Kimara, anashtakiwa kwa kutoa rushwa ya Sh 200,000.

Alidai Mei 29, mwaka huu katika maeneo ya Central Park Café iliyopo Sea View ndani ya Manispaa ya Ilala, mshtakiwa akiwa mfanyabiashara, alimpa Sh 200,000 Goodluck Mwangomango ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Sheria CCM kama kishawishi cha kupitisha mkabata wake wa upangaji.

“Mshtakiwa alikuwa anamshawishi kupitisha mkataba wake wa upangaji ambao ulikuwa unapitiwa katika kikao cha Mei 29, mwaka huu,” alidai Wakili Chimwanda.

Mshtakiwa alikana kutenda makosa hayo na akaomba adhaminiwe kwa sababu makosa yanayomkabili yanadhaminika.

Mahakama ilikubali kumpa dhamana kwa masharti ya kuwa na wadhamini wawili watakaosaini dhamana ya maandishi ya Sh milioni mbili.

Mshtakiwa alitimiza masharti ya dhamana na kesi iliahirishwa hadi Juni 24, mwaka huu kwa kutajwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles