27.2 C
Dar es Salaam
Monday, March 20, 2023

Contact us: [email protected]

G20 wajadili hatari ya uzee duniani

TOKYO, JAPAN

Kwa mara ya kwanza, watunga sera wa juu kutoka mataifa 20 yalioendelea zaidi kiuchumi (G20) wanashughulikia masuala ya kiuchumi yanayohusiana na uzee na kupungua kwa viwango kuzaa watoto.

Pia maofisa hao wanaangazia gharama za matibabu zinazoongezekana na upungufu wa wafanyakazi kwa wazee.

Mawaziri wa fedha kutoka mataifa 20 yalioendelea na yanayoinukia kichumi duniani pamoja na magavana wa Benki Kuu za mataifa hayo wanaokutana nchini Japan ambapo idadi kubwa ya wazee ni tatizo kubwa la kijamii, wameonywa kuangazia suala hilo kabla ya hali kuwa mbaya zaidi.

Waziri wa Fedha wa Japan, Taro Aso, ambaye ndiye mwenyeji wa mkutano huo, anasema kuwa cha msingi ni kwamba iwapo uzee utaanza kuonyesha athari zake kabla ya mtu kuwa tajiri, hakuna hatua zozote mwafaka zinazoweza kuchukuliwa.

Kundi hilo la G20 ni mchanganyiko wa mataifa yaliyoko kwenye ngazi tofauti za maendeleo na umri wa wakazi, kuanzia Japan ambayo wakazi wake wanazeeka kwa kasi hadi Saudi Arabia ambayo ndiyo itakayoongoza mkutano ujao wa kundi hilo na iliyo na idadi kubwa ya watu wa umri mdogo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
210,784FollowersFollow
563,000SubscribersSubscribe

Latest Articles