23 C
Dar es Salaam
Wednesday, September 18, 2024

Contact us: [email protected]

Wizara ya Ujenzi yatakiwa kuongeza kilo za mizigo kwenye boti

Ramadhan Hassan, Dodoma

Spika wa Bunge, Job Ndugai ameitaka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, kuangalia kuangalia namna ya kuongeza kilo zinazopimwa kwa abiria wanaotaka kusafiri na boti kwenda Zanzibar kutoka  kilo 20 za sasa.

Ndugai amedai kwamba kilo hizo ni ndogo hivyo iko haja ya kuliangalia upya suala hilo la mizigo kwani kilo 20 hata begi la mwanafunzi tu linafikisha , hivyo basi  liangaliwe upya ili kuondoa adha kwa wasafiri.

Awali akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Maryam Msabaha (Chadema), bungeni leo Juni 10,  Naibu Waziri Ujenzi na Uchukuzi, Elias Kwandikwa  amewataka wateja wote wanaotumia bandari kwenda Zanzibar kwa boti wahakikishe mizigo yao inapimwa kabla ya kupakiwa ili wajue kama uzito wake unastahili kutozwa ushuru.

Katika swali lake, Msabaha amedai kwamba kumekuwa na kero kubwa kwa abiria wanaotumia bandari kwenda Zanzibar kwa boti ambapo hulipishwa ushuru wa bandari kwa mizigo hata boksi la kilo 10 au mchele kg 20 kwa malipo ya Sh.9750.

” Je,ni mzigo gani ambayo abiria anapaswa kulipia ushuru huo wa bandari?,”ameuliza Msabaha.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles