23.3 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 8, 2024

Contact us: [email protected]

Mfalme Zumaridi na wenzake wasomewa maelezo ya awali

*Waendelea kusota rumande, wafuasi wake 75 waachiwa kwa dhamana

Na Clara Matimo, Mwanza

Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mwanza Machi 17 imewasomea maelezo ya awali ya mashtaka yanayowakabili washtakiwa 93 akiwemo, Diana Bundala, maarufu kama ‘Mfalme Zumaridi huku wafuasi wake 75 wakiachiwa kwa dhamana.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Doricas Akyo, ameiambia mahakama hiyo kwamba upelelezi wa kesi namba 11 na 12 inayomkabili Mfalme Zumaridi na wafuasi wake bado haujakamilika na kuiomba mahakama kupanga tarehe nyingine kwa ajili ya maelezo ya awali kusomwa.

Hakimu Mfawidhi Mwandamizi wa Mahakama ya Mkoa wa Mwanza, Monica Ndyekubora, ameahirisha kesi hiyo hadi Machi 31, mwaka huu ambapo Mfalme Zumaridi na wenzake ambao hawajapata dhamana watendelea kusota rumande.

Mfalme Zumaridi anakabiliwa na shitaka la usafirishaji haramu wa binadamu ambalo halina dhamana huku washtakiwa wengine 17 ambao ni waumini wa kanisa lake nao wakiendelea kusota naye rumande baada ya kushindwa kutumiza masharti ya dhamana ambayo ni kuwa na barua ya dhamana na kusaini bondi ya maneno ya  Sh milioni mbili.

Baada ya kuahirishwa kwa kesi hiyo wakili wa washtakiwa hao, Erick Mutta, amesema mshtakiwa mwingine ameshindwa kufika mahakamani hapo kutokana na kuugua na amelazwa  Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Ziwa Bugando(BMC) akiuguza majeraha aliyoyapata wakati wa kukamatwa na maafisa wa jeshi la polisi mkoani humo katika mtaa wa buguku jijini hapa.

“Kesi zote tatu leo ziliitwa, kesi namba 10  ya usafirishaji haramu wa binadamu ambayo inamuhusu Mfalme Zumaridi  iliitwa kwa ajili ya kutajwa  na kesi mbili zinazomkabili  pamoja na wafuasi wake ambazo ni kuzuia maofisa wa Serikali kutekeleza majukumu yao na kufanya mkusanyiko usiyo na kibali ziliitwa kwa ajili ya kusomewa maelezo ya awali.

“Lakini kwa bahati mbaya kesi hizo zote  mbili hazijaendelea kwa sababu  mshtakiwa namba 38  wa kesi namba 12 hakuweza kufika mahakamani hapa yuko hospitali kwa ajili ya matibabu na kesi nyingine ambayo inamkabili pamoja na watu wengine tisa imeshindwa kuendelea kwa kuwa  upande wa jamhuri haujakalimisha maelezo ya awali.

“Kutokana na kuugua kwa mshtakiwa huyo na kulazwa hospitali  imeshindikana kumleta mahakamani lakini tulimuombea maombi ya dhamana na mahakama ilikuwa iko radhi kwenda hospitalini kwa ajili ya kumdhaminisha  ila mpaka tunaondoka kuelekea hospitalini mdhamini alikuwa hajafika kwa hiyo utaratibu wa kumdhamini pia umeshindikana hadi wakati mwingine mdhamini atakapokuwa tayari,”amesmea wakili huyo nakuongeza

“Kesi namba 12 washtakiwa 28 wamedhaminiwa na kesi namba 11 washtakiwa sita wamedhaminiwa,”amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles