Mexico yang’ara urembo wa Dunia 2018

0
1575

Johns Njozi

Mrembo kutoka Mexico, Vanessa Ponce De Leon, ameshinda taji laurembo wa Dunia 2018  Sanya, China.

Wakati Vanessa akishinda taji la Dunia 2018 mrembo kutoka Uganga, Quiin Abenakyo, ameiwakilisha vyema Africa mashariki, kwa kutwaa taji la mrembo wa Dunia Africa.

Mrembo kutoka Tanzania, Queen Elizabeth Makune, licha ya kuchuana vikali na Mrembo kutoka Uganda, katika kipengele cha Kura hajabahatika kuingia hata 30 bora kwenye mashindano hayo.

Abenakyo, amefanikiwa kuingia kwenye 30 bora na baadae kuingia katika hatua iliyofuata ya 12 bora na kuendelea kupiga hatua kubwa zaidi mpaka kufika tano bora.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here