26.2 C
Dar es Salaam
Friday, December 3, 2021

Vyama vya upinzani vyapinga Muswada wa mabadiliko Sheria ya Vyama vya Siasa

Bethsheba Wambura, Dar es Salaam

Vyama vya Siasa 15 nchini vimesema vinapinga na vinataka mabadiliko ya Muswada wa marekebisho ya Sheria ya Vyama vya siasa uliosomwa bungeni Novemba 16, ,mwaka huu kwani una vipengele vingi vinavyovikandamiza vyama hivyo na kuwataka wabunge na wadau wa siasa kuupinga.

Akiwasilisha tamko hilo kwa niaba ya wenzake mbele ya waandishi wa habari leo Jumapili Desemba 9, jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Chama cha Ukombozi wa Umma CHAUMA) Hashim Rungwe amesema sababu kuu ya kupinga muswada huo ni kwenda kinyume na katiba ambayo imetoa uhuru kwa wanasiasa kujumuika na kufanya kazi zao pamoja lakini sheria hiyo mpya imezuia.

Amesema zuio la wanasiasa kutokufanya mikutano ya hadhara na kunadi sera zao kwa wananchi ni kinyume na sheria ya nchi kwani hata Katiba inatambua uwepo wa vyama vingi vya siasa nchini hivyo kuwazuia ni kwenda kinyume na katiba.

“Muswada huu si rafiki kwetu na tumetumia siku ya Uhuru wa nchi kudai uhuru wa vyama vya siasa ambao tumekuwa nao kwa muda mrefu hivyo hatutakubali uhodhiwe au kupokwa na mtu.
“Tunatoa wito kwa Watanzania wote bila kujali itikadi za kisiasa kupinga sheria hizi kandamizi, ” amesema.

Aidha vyama vilivuoungana ma kutoa tamko la kupinga muswada huo Ni Chama cha ACT-Wazalendo, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) , Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMA), Chama cha Wananchi (CUF), Chama cha Democratic Party ( DP), Chama cha NCCR MAGEUZI, Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC), National League for Democracy (NLD), Chama cha United People’s Democratic Party (UPDP) na Chama cha Kijamii (CCK).

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,848FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles