23.3 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

MERKEL AJIBU TUHUMA ZA RAIS WA UTURUKI

UJerumani


KANSELA wa Ujerumani, Angela Markel, amesema tuhuma zilizotolewa dhidi yake na Rais wa Uturuki, Recep Erdogan, kuhusu kuwaunga mkono magaidi hazina msingi wowote.

Msemaji wa Kansela wa Ujerumani, Steffen Seibert,  alibainisha kwamba Angela Merkel hana nia ya kushiriki katika michezo ya fitina.

Rais Erdogan wa Uturuki juzi alimtuhumu Merkel kuwa anawaunga mkono magaidi, anawaficha nchini kwake na kukwamisha mapambano dhidi ya ugaidi.

Siku za hivi karibuni maafisa wa miji kadhaa ya Ujerumani walifuta vikao vya uchaguzi vya maafisa wa chama tawala cha Uturuki, hatua iliyoikasirisha serikali ya Erdogan.

Rais wa Uturuki amelinganisha hatua hiyo ya kufutwa vikao hivyo kuwa ni sawa na hatua za utawala wa Kinazi. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles