24.7 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 19, 2024

Contact us: [email protected]

Mechi Simba, Yanga kupangiwa tarehe mpya Waziri kuipatanisha Yanga na TFF

Na Winfrida Mtoi
Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Innocent Bashungwa, amekutana na viongozi wa taasisi za soka nchini, kujadili sakata la kuahirishwa mchezo wa Simba na Yanga na kukubaliana kurudiwa kwa mechi hiyo.

Mchezo huo ulikuwa uchezewe Mei 8, 2021 kwenye uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam, hivyo Bashungwa kuziachia majukumu Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Bodi ya Ligi Kuu kukaa na kupanga tarehe mpya ya mechi hiyo kupigwa.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano Serikalini, John Mapelele, kutokana na maagizo yaliyotolewa Bungeni jana na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, usiku huo huo Waziri Bashungwa alifanya kikao cha mashauriano na pande husika.


Katika kikao hicho, kilichohudhuriwa na viongozi wa Simba na Yanga, TFF na Bodi ya Ligi, Baraza la Michezo la Taifa(BMT)na wizarani.
Viongozi waliohudhuria ni Rais wa TFF, Wallace Karia na Katibu Mkuu, Wilfred Kidau, Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi, Stephen Mguto na Mtendaji wake, Almas Kasongo.


Simba iliwakilishwa na Mwenyekiti wa Klabu, Murtaza Mangungu na Mtendaji Mkuu, Barbara Gonzalez na Mjumbe wa Bodi ya Klabu, Zacharia Hanspoppe, huku Yanga ikiongozwa na Mwenyekiti Dk Mshindo Msolla, Mjumbe wa Kamati Tendaji, Bahati Mwaseba na Kaimu Katibu Mkuu Haji Mfikirwa.


Waziri Bashungwa amewaomba viongozi wa klabu na mashabiki kuwa watulivu na kuamini Serikali ilikuwa na nia njema na sababu za msingi iliposhauri mechi isogezwe mbele kabla ya kujitokeza mazingira yaliyosababisha Bodi ya Ligi kulazimika kuuahirisha.


“Mashabiki waliokata tiketi waziri ameagiza kituo cha Kitaifa cha Data (Data Center) wanaosimamia mfumo wa N-Card kuwarejeshea mashabiki wote 43, 947,tiketi zao kwenye mfumo wa kadi za kuingilia uwanjani ili tiketi hizo za kielektroniki ziwasaidie kuingia tena uwanjani kwa kila mmoja kukaa eneo lile lile alilokata awali kwenye mchezo wa marudiano,”.


Pia mfumo wa N-Card uruhusu kuuzwa tiketi zaidi kwa mashabiki wapya watakaoamua kuingia uwanjani siku hiyo hadi kufikia au kukidhi idadi inayoruhusiwa kulingana na uwezo uwanja
Aidha taarifa hiyo ilieleza kuwepo sintofahamu na kutokuaminiana kati ya baadhi ya klabu hususani Yanga na TFF kuendelea licha ya vikao vya kuiondoa kufanyika.


Kutokana na jambo hilo, waziri ameahidi kuitisha kikao kingine haraka kati ya pande hizo mbili ili kujadili changamoto na kuondoa hali iliyopo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles