24.4 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

Kila Mtanzania anajukumu la kulinda Amani- Alhaji Mussa

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

SHEIKH wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhaj Mussa Salum amesema kila Mtanzania anajukumu la kuilinda amani na kuimarisha umoja wa kitaifa uliopo kwa kuhakikisha hakuna mtu anayeweza kusababisha uvunjifu au mfarakano katika nchi.

Wito huo umetolewa Mkoani Dar es Salaam na Sheikh wa mkoa wa Dar es Salaam, Alhaj Mussa Salum wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ibada ya sikukuu ya Eid Firtri ambapo kitaifa inaswaliwa katika viwanja vya mnazi mmoja Mkoa wa Dar es salaam.

Alisema amani iliyopo kwa sasa inapaswa kuendelea hivyo ni jukumu la kila mmoja kuilinda na kushirikiana na serikali katika kutokomeza vitendo vya uhalifu na uvunjifu wa amani ya nchi.

“Sisi kama Baraza la Waislamu mkoa wa Dar es salaam tunuunga mkono kauli ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Hassan Suluhu aliyoitoa hivi karibu ya kwa kuhakikisha kila familia inalinda amani na kuimarisha umoja wa kitaifa”alisema Sheikh Alhaj Salum

Akizungumzia kuhusiana na ibada ya Sikukuu ya Eid Fitri kitaifa mwaka huu inafanyika mkoa wa Dar es salaam katika viwanja vya karimjee.

Alisema katika ibada hiyo kutaudhuliwa na viongozi mbalimbali wa nchi , mabalozi akiwemo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Khasimu Majaliwa Khasimu, huku katika baraza la Eid mgeni rasmi akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Hassan Suluhu

“Hii ni heshima kwetu sisi kama baraza la Waislamu wa Dar es salaam tumefarijika sana kuwa wenyeji wa ibada ya swala
Eid Fitri kwa mwaka 2021 sawa na mwaka 1442 Hijiria kuswaliwa katika mkoa wetu”alisema

Aidha amewataka waumini wa dini ya Kiislamu kujitokeza kwa wingi katika ibada hiyo maalumu ya kumshukuru Mungu kwa ajili ya kumaliza mfungo wa Ramadhani salama.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles