25.2 C
Dar es Salaam
Friday, September 17, 2021

McGregor atangaza kustaafu ngumi

 DUBLIN, IRELAND 

BINGWA wa mchezo wa ngumi wa UFC, Conor McGregor, amewashangaza mashabiki baada ya kutangaza kustaafu mchezo huo huku akiwa na umri wa miaka 31. 

Nyota huyo raia wa nchini Ireland, juzi asubuhi alitumia ukurasa wake wa Twitter na kutangaza kuwa hana mpango wa kupigana tena. 

“Helo watu wangu, nimeamua kustaafu kupigana. Asanteni wote kwa kumbukumbu niliyokuwa nayo pamoja, hii ni picha nikiwa na mama yangu huko Las Vegas, nikiwa nimechukua moja kati ya mataji yangu makubwa duniani. 

“Nilifanikiwa kwenda na taji hilo la ndoto yangu hadi nyumbani, niseme nawapenda sana, lakini chochote unachokifikiria ndio hicho hicho,” aliandika. 

Bingwa huyo ambaye anafahamika kwa jina lingine la The Notorious One, awali alitangaza mwaka huu yupo kwenye mipango ya kupigana na mkongwe Anderson Silva, Jorge Masvidal pamoja na kurudia pambano dhidi ya Khabib Nurmagomedov, lakini kwa taarifa hiyo hakutokuwa na pambano tena. 

Kikubwa kilicho washangaza mashabiki ni kuona bondia huyo wa ngumi mchanganyiko akistaafu wakati ndio anaanza kupata fedha nyingi kwenye maisha ya mchezo huo. Anatajwa kuingiza kiasi cha dola milioni 100 kutokana na mapambano yake ya hivi karibuni. 

Hata hivyo hii sio mara ya kwanza kwa bondio huyo kutangaza kustaafu ngumi, Machi mwaka jana alitangaza kustaafu lakini akaja kubadilisha maamuzi yake kabla ya Desemba. 

Baada ya kutangaza kurudi alishuka ulingoni Januari mwaka huu kupambana na Donald Cerrone ‘Cowboy’ na kufanikiwa kushinda katika sekunde ya 40 katika uzani wa welterweight. 

Mashabiki wanaamini bondia huyo anaweza kubadili maamuzi tena japokuwa aliwahi kusema anataka kustaafu akiwa na umri mdogo. 

Katika historia ya ngumi zake za kulipwa amefanikiwa kupigana mapambano 26, akishinda mara 22, kati ya hayo alishinda 19 kwa KO na kupoteza manne. 

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
156,567FollowersFollow
517,000SubscribersSubscribe

Latest Articles