23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Maandamano makubwa ya kupinga ubaguzi yafanyika

 WASHINGTON, MAREKANI

MAANDAMANO makubwa ya amani yamefanyika kote nchini Marekani kupinga ubaguzi wa rangi na unyanyasaji unaotekelezwa na maafisa wa polisi ikiwa ni siku ya 12 ya maandamano yaliosababishwa na kifo cha George Floyd.

Makumi ya maelfu ya watu waliandamana mjini Washington DC ikiwa ndio maandamano makubwa kufanyika katika mji huo kufikia sasa.

Makundi ya watu pia yaliandamana mjini New York, Chicago, LA na San Fransisco. Wakati huohuo , watu walitoa heshima zao kwa Floyd katika jimbo la North Carolina, ambapo alizaliwa kabla ya ibada ya kumbukumbu yake kufanywa.

Floyd, mtu mweusi ambaye hakuwa na silaha, alifariki katika mikono ya polisi katika mji wa Minneapolis Mei 25, 2020. 

Picha ya video ilimuonesha ofisa wa polisi ambaye ni mzungu akiwa ameweka goti lake kwenye shingo ya Floyd kwa zaidi ya dakika tisa akiwa amekandamizwa barabarani.

Ofisa huyo wa polisi, Derek Chauvin amefukuzwa kazi na kushtakiwa kwa kutekeleza mauaji. Maofisa wengine watatu ambao walikuwepo katika eneo hilo pia walifutwa kazi na kushitakiwa kwa kusaidia na kuunga mkono kilichokuwa kikiendelea.

Maandamano makubwa ya kupinga ubaguzi wa rangi pia yalifanyika katika baadhi ya mataifa mengine. 

Nchini Uingereza, katika bustani ya bunge katikati ya mji wa London, kulikuwa na watu wengi licha ya wito wa serikali kutokongamana kwa hofu ya kusambaa kwa virusi vya corona.

Nchini Australia, kulikuwa na maandamano makubwa katika miji ya Sidney na Melbourne na Brisbane yaliyoangazia jinsi raia wenye chimbuko la Australia walivyokuwa wakinyanyaswa. Pia kulikuwa na maandamano nchini Ufaransa, Ujerumani na Uhispania.

Maandamano makubwa zaidi yalifanyika mjini Washington DC ambapo waandamanaji waliokuwa wakibeba mabango yalioandikwa ‘Black Lives Matters’ walikongamana kwa amani karibu na mji mkuu, katika eneo la kumbukumbu la Lincoln na nje ya bustani ya Lafayette , karibu na ikulu ya Whitehouse karibu na jumba jipya kwa jina Black Lives Matter Plaza.

Meya Muriel Bowser aliwakaribisha waaandamanaji akisema kuwa watu hao walituma ujumbe kwa Rais Donald Trump.

“Iwapo anaweza kuzuia chochote kufanyika Washington DC basi anaweza kufika katika jimbo lolote na hakuna hata mmoja wetu atakayekuwa salama. Wanajeshi wetu hawafai kutumiwa jinsi hii hawafai kutakiwa kuwasukuma raia wa Marekani,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles