28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Array

Waliokufa kwa Covid-19 wapindukia 400,000

 BRUSSELS, UBELGIJI

SERIKALI ya Brazil imesema imesimamisha zoezi la kuchapisha idadi ya watu waliokufa kwa Covid -19 au waliopata maambukizi ya virusi vya corona nchini humo, hukutaarifa kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) likieleza kuwa idadi ya waliokufa kwa ugonjwa hio wamevuka 400,000 duniani.

Hatua hiyo ya Brazili inakwenda kinyume na mapendekezo ya WHO huku nchi hiyo kwa sasa ndio ina idadi kubwa ya vifo na maambukizi ya virusi vya corona katika nchi za Amerika ya Kusini.

Wakati huo huo, madereva wa malori ambao ni miongoni mwa watoa huduma muhimu barani Afrika wamesema wanakabiliwa na unyanyapaa tangu kuzuka janga la maambukizi ya virusi vya corona. 

Kundi la watu hawa husafirisha bidhaa kama chakula, mafuta, vifaa na mahitaji mengine muhimu wakati mwingine wanapitia kwenye barabara zenye hatari hasa wakati huu ambapo ulimwengu unakabiliwa na hali ngumu ya kiuchumi. 

Madereva wa malori barani Afrika wanalalamika kuwa wao ndio wanatuhumiwa kwa kusambaza maambukizi ya virusi vya corona.

Ni kweli mamia ya madereva hao wa malori wameambukizwa virusi hivyo katika wiki za hivi karibuni, wanatoa malalamiko yao kwamba wananyanyaswa na kuchukuliwa kama wahalifu na mara nyingine wakikamatwa na maofisa wa serikali hali ambayo inasababisha adha kwenye usafirishaji wa mizigo na kufanya shughuli za barabarani ziende polepole kutokana na misongamano ya magari hayo ya kubeba mizigo.

 Hali hiyo imeibua changamoto kwa serikali nyingi kwenye nchi za Afrika zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara, ambapo mipaka mingi bado imefungwa kutokana na janga la corona, nchi hizo pia zinapambana juu ya jinsi ya kuyadhibiti maambukizi na kuendelea kwa shughuli za biashara. Nchi za Afrika mashariki zinajitahidi kufikia makubaliano ya pamoja.

Mamlaka za afya katika nchi za Afrika Mashariki bado hazina vifaa vya kutosha vya kupimia watu na hivyo basi zinategemea simu yz rununu za madereva wa malori kama njia moja wapo ya kuwafuatilia.

Pontiano Kaleebu, anayeongoza Taasisi ya Utafiti wa Virusi nchini Uganda alisema kuweka mkazo na kufuatilia kwa karibu maeneo yanayodhaniwa kuwa na maambukizi ya kiwango kikubwa sio hatua za kibaguzi hata kidogo bali ni kutokana na hali halisi ilivyo.

Kwa upande wake Aggrey Keya, mtaalamu wa maabara kwenye eneo la mpaka wa Namanga alisema shughuli za upimaji kwenye mpaka mara nyingi huenda polepole, na changamoto ni idadi kubwa ya watu wanaofika mpakani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles