25.2 C
Dar es Salaam
Sunday, December 4, 2022

Contact us: [email protected]

Mbunge Chadema amkingia kifua Magufuli

japhary-michaelNa UPENDO MOSHA- MOSHI

MBUNGE wa Moshi Mjini, Japhary Michael (Chadema), amewataka wananchi wampe muda Rais Dk. John Magufuli ili kutekeleza ahadi ya kufufua viwanda.

Michael aliyasema hayo jana alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara, huku akisikiliza kero za wananchi katika Viwanja vya Pasua Sokoni, mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro.

“Hampaswi kumlalamikia rais katika kipindi hiki, bali wajibu wenu ni kuipa muda Serikali ili iweze kutekeleza ahadi zake.

“Wananchi wengi wamekuwa wakilalamika juu ya kusuasua katika utekelezaji wa sera ya ufufuaji wa viwanda katika maeneo mbalimbali nchini hususani mkoani Kilimanjaro na kumtupia lawama rais jambo ambalo si sahihi,” alisema Michael.

Kuhusu ufufuaji wa viwanda mkoani Kilimanjaro, mbunge huyo alisema tayari ameshawasiliana na waziri mwenye dhamana ya viwanda na kufikia makubaliano.

“Nimeongea na waziri mwenye dhamana ya viwanda na ameonyesha nia kabisa ya kufufua viwanda vyetu hapa mjini na mkoa mzima kwa ujumla.

“Kazi iliyobaki ni kusubiri utekelezaji wa ahadi hii na nyingine nyingi ambazo Serikali iliahidi kwenu wananchi,” alisema mbunge huyo.

Akizungumzia mchakato wa Mji wa Moshi kupandishwa hadhi na kuwa Jiji, alisema tayari hatua mbalimbali zimeshachukuliwa na Serikali imeshatangaza katika Gazeti la Serikali la kuainisha mipaka.

Naye Meya wa Manispaa ya Moshi, Raymond Mboya, alisema vitongoji 40 vilivyohamishwa kutoka katika wilaya za Hai na Moshi Vijijini, vimeingizwa katika mamlaka ya kiutawala baada ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, kusaini sheria hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,538FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles