24.8 C
Dar es Salaam
Saturday, May 28, 2022

Uchangiaji damu wahusishwa na ushirikina

damuNa Odace Rwimo, Tabora

WAKAZI wa Manispaa ya Tabora wameshauriwa kujenga utamaduni wa kujitolea kuchangia damu kwa hiari, ili kuokoa maisha ya wananchi wanaopoteza maisha kila siku kwa kukosa damu.

Wito huo ulitolewa jana katika mdahalo maalumu ulioandaliwa na Kituo cha Redio cha CG FM cha mjini Tabora ukilenga kuhamasisha zoezi la uchangiaji damu kwa hiari.

Akizugumza katika mdahalo huo, Meneja Vipindi wa CG FM, Winfrida Celestine alisema kituo chake kimeamua kuendesha kampeni hiyo baada ya kubaini uwepo wa upungufu mkubwa wa damu safi na salama katika
zahanati, vituo vya afya na hospitali za mkoa huo.

Alisema jitihada za haraka zinapaswa kuchukuliwa na wadau wote ili kuelimisha jamii athari za kutokuwa na damu ya kutosha katika vituo vya kutolewa huduma za afya na umuhimu wa jamii kujitolea kuchangia damu ili kuepusha vifo zaidi.

“Takwimu zinaonyesha kwa mwezi mmoja tu Mkoa wa Tabora unahitaji chupa za damu salama zenye ujazo wa mm 400 zaidi ya 2300 ili kukabiliana na changamoto inayowakabili wajawazito na wanaopata ajali za
barabarani,”alisema.
Katika mdahalo huo baadhi ya wadau wakiwemo wanafunzi wa sekondari na vyuo ambao walisema watu wamekuwa wakishindwa kujitolea damu kwa  kile kinachodaiwa hupunguza  madini mwilini na kuhisi kizunguzungu.

Wadau Frank John, Patrik Shigela  kutoka  Chuo cha Utumishi wa Umma Tabora, Ambane Liundi  kutoka  Chuo cha Musoma Utalii na Silvester Nyawaliko  kutoka  Kaze

Hill sekondari walisema baadhi ya watu wanadai ukitoa damu lazima upatwe na kizunguzungu  jambo linalosababisha kukwepa uchangiaji.

Aidha walisema baadhi huhofia kuchangia damu kutokana na  imani kuwa huenda inaenda kufanyiwa mambo ya kishirikina au kuuzwa kwa watu wenye uhitaji.

Hata  hivyo katika mdahalo huo , baadhi ya  watu  waliokwisha changia damu zaidi ya mara tatu  walisema  madai ya wananchi hayo hayana ukweli kwani tangu waanze kujitolea damu hawajapata athari yoyote.

Meneja wa Benki ya Damu Salama Kanda ya Magharibi, Dk. Ipyana Kiganuka alisema kazi ya kuchangia damu halina madhara yoyote kwa mchangiaji ila mchangiaji anapaswa kupewa elimu na maelekezo ya nini afanye baada ya kuchangia.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
192,577FollowersFollow
541,000SubscribersSubscribe

Latest Articles