23.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 8, 2021

Mbunge amtaka Rais Kenyatta afukuze mawaziri wavivu

NAIROBI, KENYA

MBUNGE wa Kieni, Kanini Kega amemtaka Rais Uhuru Kenyatta kuwafukuza mawaziri wanaomkwamisha katika utekelezaji wa miradi yake ya Ajenda Kuu Nne.

Kega alisema sehemu ya mawaziri hawafanyi kazi, hivyo kuwa ngumu kwa Rais kutimiza ahadi alizotoa kwa Wakenya wakati wa Uchaguzi Mkuu wa 2017.

Akizungumza mjini Nyeri Jumatatu wiki hii, mwakilishi huyo wa Kieni alisema Rais Kenyatta mara nyingi amekuwa akilalamika utendaji wa baadhi ya mawaziri.

Alitoa mfano wa mwishoni mwa wiki wakati Kenyatta alipowaonya mawaziri dhidi ya uendekezaji siasa kabla ya 2022 wakati alipoonana nao Ikulu.

“Sehemu kubwa ya mawaziri hawafanyi kazi kama walivyotarajiwa na Wakenya na kumkatisha tamaa Rais. Wanapaswa kujiuzulu badala ya kusubiri kufukuzwa,” alisema Kega.

Mbunge huyo alisema Bunge la Taifa, ambalo linadhibitiwa na Chama tawala cha Jubilee, litamuunga mkono Rais iwapo atahitaji msaada wa kufanya mabadiliko ya baraza lake la mawaziri.

Aliongeza kuwa kwa vile Rais amebakiwa na miaka mitatu tu kutekeleza ahadi zake, anahitaji timu yenye dhamira ya dhati.

Miradi mikubwa aliyopanga inahusisha uzalishaji, huduma za afya, nyumba nafuu na usalama wa chakula.

“Rais amebakiwa miaka mitatu tu kutimiza ahadi alizotoa kwa Wakenya. Akikosa timu imara ya kumsaidia, atakabiliwa na changaoto katika kuzitekeleza,” alisema mtunga sheria huyo.

Kwa mujibu wa Kega, nusu ya Baraza la Mawaziri ni dhaifu huku wengine hawafahamu majukumu yao. Hivyo wale walioshindwa wawapishe Wakenya wengine wenye uwezo waitumikie serikali.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
168,549FollowersFollow
527,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles