26.3 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 30, 2021

Mawaziri kulipwa mishahara maishani DRC

KINSHASA, DRC

SERIKALI ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) imetetea uamuzi wake wa kuruhusu mawaziri kulipwa mishahara na marupurupu kwa maisha yao yote.

Katika taarifa iliyotolewa juzi, serikali imesema malipo hayo si ya kuwatajirisha maafisa hao waandamizi.

Maagizo mawili, yanayoruhusu mawaziri kupokea marupurupu ya kiwango cha chini cha dola 2,000 sawa na Sh milioni 4.6 yameshutumiwa kwa kiasi kikubwa.

Hiyo inatokana na ukweli kwamba idadi kubwa ya raia nchini Congo wanaishi katika umaskini uliotopea.

Serikali iliyoondoka ilikuwa inawapatia mawaziri kiwango cha chini kuwatosheleza mahitaji yao ya kimsingi, kama chakula, makazi na huduma ya afya.

Malipo hayo ni ya kuwaepusha kuishia katika umaskini”, taarifa inasema.

Maagizo mawili yaliyotiwa saini na Waziri Mkuu anayeondoka Bruno Tshibala Novemba mwaka jana yamekuja ripotiwa kwa kiasi kikubwa hivi karibuni.

Agizo la kwanza linawapa mawaziri wakuu mishahara ya kila mwezi sawa na asilimia 30 ya mshahara anaopokea sasa waziri mkuu.

Aidha wanajihakikishia tiketi ya mara moja ya ndege kwa mwaka na marupurupu ya nyumba yenye thamani ya dola 5,000 (Sh milioni 11).

Agizo la pili linawapa mawaziri mishahara sawa na asilimia 30 ya wanayopokea mawaziri wa sasa na dola 1,000 kila mwezi kulipia makazi.

Aidha watapokea pia tiketi ya mara moja kwa mwaka ya ndege, Reuters linaripoti.

Mshauri wa Rais wa zamani Joseph Kabila amesema maagizo hayo ‘hayaendani na mtazamo wetu wa kiuchumi na kijamii”.

Mshauri huyo, Patrick Nkanga ameandika kwenye mtandao wa Twitter: “Ni kupita kiasi na ni gharama kubwa zisizo na msingi za upotevu wa fedha za umma.”

Lakini serikali imetetea maagizo hayo na kueleza kwamba hayatowalenga mawaziri wa awamu iliyopita, bali walioko sasa serikalini na serikali zijazo.

Rais mpya wa Jamhuri ya Kidmeorasi ya Congo, Felix Tshisekedi, aliapishwa madarakani mwezi uliopita.

Alipokea wadhifa huo kutoka kwa Kabila katika makabidhiamo ya kwanza ya madaraka yaliyofanyika kwa amani katika nchi hiyo na uliowahi kushuhudiwa katika miaka 60.

Hata hivyo, matokeo ya uchaguzi yalishutumiwa huku kukiwa na ripoti za makubaliano kati ya Rais Kabila na Tshisekedi, hata hivyo pande zote zilikana tuhuma hizo.

Katika ripoti ya hivi karibuni ya Transparency International 2017 kuhusu viwango vya rushwa, DRC iliorodheshwa ya 161 kati ya nchi 180 duniani zinazoongoza kwa rushwa.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,451FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles