22.2 C
Dar es Salaam
Monday, October 14, 2024

Contact us: [email protected]

MBUNGE AHOJI UHALALI WA KIAPO CHA MTULIA, DK. MOLLEL

Na Fredy Azzah, Dodoma

Uchache wa wabunge waliohudhuria Mkutano wa 11 ulioanza leo mjini Dodoma, umemtisha Mbunge wa Ulanga, Goodluck Mlinga (CCM), ambapo amehoji endapo kiapo cha wabunge wapya wa Chama Cha Mapinduzi Dk. Godwin Mollel (Siha) na Mauld Mtulia (Kinondoni) walioapishwa leo ni halali ama la.

Leo wakati wabunge hao wakila kiapo cha uaminifu mbele ya Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson, wabunge wa upinzani waliokuwamo bungeni ni takribani wanne tu wa Chama cha Wananchi (CUF).

Mlinga amehoji hayo baada ya kipindi cha maswali na majibu, Mlinga akiomba mwongozo wa Spika, kama kiapo cha wabunge hao ni halali kwa sababu wameapa huku wabunge wakiwa nusu idadi yao.

Aidha, amehoji pia endapo wabunge walioudhuria bunge hilo watalipwa posho kwa sababu ya akidi kutotimia na ni hatua gani zitachukuliwa kwa wale ambao hawakuhudhuria.

Akijibu mwongozo huo, Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia amesema: “Mlinga kauliza kuhusu akidi, kwa sababu anasema kikanuni inatakiwa wabunge wawe nusu, lakini kanuni ya 77 (1-5), inasema kuhusu shughuli za uendeshaji wa Bunge na akidi.

“Akisema akidi haijatimia sijui yeye ndiyo kahesabu hao wabunge ama vipi, niseme tu suala la akidi ni wakati wa kuanza kikao kwa hiyo mwongozo anaoutaka sasa haupo kikanuni, kwa hiyo walioapishwa wameapishwa kihalali”.

Pamoja na wabunge hao wanne wa CUF, walikuwapo wabunge wawili wa Chadema ambao ni Serengeti, Chacha Marwa na Joyce Sokombi wa Viti Maalumu.

Hadi kipindi cha maswali na majibu kinakwisha, wabunge wa upinzani walikuwa 18 huku pia wa CCM wakiwa takribani nusu ya idadi yao. Idadi hiyo iliendelea kubaki hivyo hadi Bunge linaahirishwa saa saba mchana huku mawaziri na manaibu waziri waliokuwa wameketi kwenye viti vyao walikuwa chini ya 10.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles