Mazishi ya msanii Mbalamwezi kusubiri kibali cha polisi

0
1164

Jeremiah Ernest, Dar es Salaam.

Taratibu za mazishi ya msanii wa Kundi la The Mafik, Mbalamwezi ambaye mwili wake ulikutwa maeneo ya Mbezi Afrikana jijini Dar es Salaam zinasubiri kibali kutoka polisi kabla kabla ya kuzikwa.

Mwili wa msanii huyo ambaye msiba wake uko maeneo ya Temeke jijini Dar es Salaam, uliokotwa maeneo hayo juzi, ukiwa hauna nguo huku ukiwa na majeraha yanayodhaniwa yametokana na kipigo.

Taarifa kutoka kwa ndugu wa karibu zinadai kuwa msanii huyo aliondoka nyumbani siku tatu zilizopita ambapo siku ya pili simu na gitaa lake viliokotwa na msamaria mwema mbezi Jogoo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here