26.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, October 27, 2021

MATUMIZI YA DOLA KWENYE UCHUMI YAATHIRI SHILINGI

Na Mwandishi Wetu


 

Suala la matumizi ya Dola za Marekani kama mbadala katika uchumi wa Tanzania, linatatiza wengi na wataalamu wamegawanyika kwa kukosa msimamo wa pamoja kuhusu tatizo hilo.

Lakini ni ukweli usiopingika kuwa matumizi ya Dola yanaweza kusababisha matatizo kadhaa katika uchumi wa Taifa husika. Mojawapo ni kupoteza thamani kwa sarafu ya shilingi na kujitokeza kwa tabia ya kuthamini Dola ya Marekani kuliko Shilingi ya Tanzania katika baadhi ya miamala muhimu. Heshima kwa nchi huru yenye sarafu yake hupungua kwani utawala ni pamoja na kuwa na sarafu yenu. 
Hivi leo uchumi wa Venezuela unayumbishwa kwa matatizo yatokanayo na hali hiyo.

Wahusika hulazimika kuweka bei katika Dola ili kujilinda na kupoteza fedha na thamani ya biashara zao, kwani Shilingi inashuka thamani kiholela sana. Wakizibadili kuwa Dola huwawezesha kununua bidhaa nyingine nje ya nchi bila kupoteza thamani yake. 
 
Kwa maelezo ya msomi wa uchumi, Profesa Honest Ngowi, ni kwamba nia kuu ya kuweka bei katika Dola ni kulinda thamani ya biashara. Hata hivyo, hii inakuwa lazima tu kwa sababu ya kuyumba sana kwa thamani ya Shilingi ikilinganishwa na Dola sokoni.

Anasema tatizo jingine ni nchi kutoweza kusimamia sera zake za fedha vizuri na fedha za nchi nyingine ndizo zinatamalaki katika mzunguko na miamala ya nchi husika. Ndiyo maana ni lazima kutafuta suluhu ya kudumu ya tatizo hili.
Wakati mwingine ni kukithiri kwa rushwa na utakatishaji wa fedha haramu katika uchumi, kwani huhitaji matumizi ya sarafu za nje na za ndani zishiriki kwa pamoja. Mapato ya bidhaa kama madawa ya kulevya huendeshwa katika mfumo wa sarafu mbili ndani na nje ya nchi.
Prof Ngowi anasema mambo mengi yanapaswa kufanyika ili kuwa na suluhu endelevu kwani kuzuia hali hii kwa sheria tu si mwafaka.

Jawabu ni kuimarisha thamani ya Shilingi kwa nchi kupata fedha nyingi za kigeni baada ya kuuza bidhaa na huduma nje.

Mazingira rafiki na wezeshi yanahitajika katika uchumi  husika.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
163,388FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles