28.2 C
Dar es Salaam
Sunday, October 2, 2022

MATAJIRI TANZANITE WAITWA IKULU

Na Masyaga Matinyi,Mirerani


 

WAMILIKI wa migodi na wafanyabiashara wakubwa (masterdealers) wa madini ya tanzanite, wameitwa mbele ya timu ya Serikali ya majadiliano Ikulu, Dar es Salaam kesho.

Kwa mujibu wa barua iliyosainiwa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi, Juni 28, 2018 kwenda kwa wadau hao (MTANZANIA imeiona nakala), wametakiwa kuzingatia wito huo na kufika mbele ya timu hiyo saa 4 asubuhi.

Sehemu ya barua hiyo imesema; “Kama unavyofahamu, Serikali kupitia timu ya Serikali ya majadiliano imekuwa katika majadiliano na wawakilishi wa makampuni ya uchimbaji wa madini hapa nchini.

“Madhumuni ya majadiliano hayo ni kuangalia taratibu za uchimbaji, uendeshaji wa kampuni na biashara ya madini husika kulingana na Sheria ya Madini ya mwaka 2010, kama ilivyoboreshwa mwaka 2017.”

Taarifa zinazotakiwa kuwasilishwa mbele ya timu ya Serikali kwa mujibu wa leseni ndogo ya uchimbaji madini (Primary Mining Licence – PML), ni pamoja na zinazoeleza uendeshaji wa eneo la mgodi na uchimbaji wa madini unaozingatia utafiti na mpango wa uchimbaji ulioidhinishwa wakati wa kupewa leseni.

Kwa habari kamili jipatie nakala ya gazeti lako la MTANZANIA hapo juu

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,474FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles