23.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

RAIS MAGUFULI AWASHANGAA WANAOMKATISHA TAMAA

NORA DAMIAN Na ANDREW MSECHU,DAR ES SALAAM


 

RAIS John Magufuli amesema anashangazwa na watu wanaojaribu kumkatisha tamaa akisema kuwa yote anayoyafanya katika utawala wake ni kwa manufaa ya watanzania wote.

Akizungumza katika uzinduzi wa kitabu cha Mwenyekiti wa Kampuni za IPP, Dk. Reginald Mengi jijini Dar es Salaam jana, alisema amebaini kukatishwa tamaa ndani ya Serikali ni kukubwa kuliko alivyotarajia awali kabla hajawa rais.

“Kabla sijawa Rais nilidhani kwamba ukishakuwa katika nafasi hiyo hakuna anayeweza kukukatisha tamaa, lakini ninayokutana nayo ni tofauti na niliyokuwa nikifikiria. Kukatishwa tamaa ndani ya Serikali ni kukubwa sana,” alisema Rais Magufuli.

Alisema kitabu hicho kilichopewa jina ‘I can, I must, I will’ kinachoelezea kwa sehemu kubwa maisha ya mfanyabiashara huyo maarufu na changamoto alizokutana nazo, kinampa funzo kuhusu namna ya kukimbilia mafanikio na namna ya kutatua vikwazo mtu anavyokutana navyo katika kufikia mafanikio anayoyahitaji.

Alisema iwapo Watanzania wataukataa umasikini kwa pamoja wakijiamini na kuwa na uamuzi thabiti wanaweza watafanikiwa, hivyo kuwataka wote wanaojaribu kukatisha tamaa wengine waache.

Rais Magufuli alisema anakumbuka namna ambavyo baadhi ya watu serikalini waliwahi kukejeli na kujaribu kuwakatisha tamaa Watanzania kwamba hawawezi kuwekeza kwenye gesi Mtwara kwa sababu hawana mitaji ya kuendesha uwekezaji huo huku wakijua kwamba iwapo Watanzania watapewa nafasi wanaweza kufanya mambo makubwa.

Alisema ameshuhudia watu wanaweza kukatishwa tamaa kuanzia ngazi ya mtu binafsi, familia na hata serikalini, lakini yeye ameamua kusimamia kile anachoamini kwamba ni kwa manufaa ya Watanzania wote.

Kwa habari kamili jipatie nakala ya gazeti lako la MTANZANIA hapo juu

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles