24.2 C
Dar es Salaam
Monday, September 26, 2022

BUNGE LASUBIRI FAMILIA MAZISHI YA MAJIMAREFU

| Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Ofisi ya Bunge imesema inasubiri kukutana na familia kupanga mazishi ya aliyekuwa Mbunge wa Korogwe Vijijini, Stephen Ngonyani maarufu Profesa Majimarefu, aliyefariki dunia katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), usiku wa kuamkia leo.

Akizungumza na Mtanzania Digital leo Jumanne Julai 3, Katibu wa Bunge, Stephen Kagaigai amesema ni kawaida kwa Ofisi ya Bunge kugharamia mazishi lakini kwa kuwa msiba ndiyo kwanza umetokea, wanasubiri kukutana na familia kwanza.

“Msiba ndiyo kwanza umetokea, inabidi tukutane na familia tuzungumze, waamue mahala wanapotaka kuzika na vitu kama hivyo, ni lazima tushirikiane,” amesema Kagaigai.

Aidha, akimzungumzia marehemu Profesa Majimarefu, Kagaigai amesema; “marehemu alikuwa mtu mzuri mcheshi, mchangamfu, anapenda ushirikiano na utani.

“Lakini pia kwa muda mfupi niliofanya kazi naye, nimemuona kama ana mapenzi na nchi, alikuwa mzalendo kweli kweli.”

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,044FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles