22.6 C
Dar es Salaam
Sunday, May 5, 2024

Contact us: [email protected]

Mashindano ya vijana ‘Just Fit Inter Schools kurindima Disemba 9

Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital

Mashindano ya vijana yanayoitwa ‘ Just Fit Inter Schools Games’, yanatarajia kufanyika Disemba 9-10, 2023 yakihusisha michezo mitano tofauti itakayofanyika kwenye viwanja vya Gymkhana, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Novemba 20, 2023 leo Dar es Salaam,  Meneja masoko wa Just Fit , Jabir Jabir amesema michezo itakayokuwepo  katika mashindano hayo ni kikapu, soka, chess, kuogelea na tenisi, lengo likiwa ni kukuza vipaji  na kuwajengea vijana tabia ya kupenda michezo.

Amesema mashindano hayo yanafanyika kwa mara ya kwanza lakini yatakuwa yakifanyika kila mwaka kuanzia sasa  ili kuibua vipaji  ambayo baadaye vitakuwa  juu kama kina  Hashim Thabit, Mbwana Samatta, Fei Toto, John Bocco na wengine wanaofanya vizuri kitaifa na Kimataifa.

Mkurugenzi wa  mradi wa Justfit Foundation, Begam Sykes.

‘Lengo la kuanzisha ‘Just Fit Inter Schools Games’ ni kujenga tabia ya kupenda michezo kwa vijana/watoto. Ili kuunga mkono juhudi za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika jitihada zake za kukuza vipaji vya michezo kuanzia rika la chini, yaani kwa watoto au vijana wadogo.

Amewaomba wadhamini wengine wataka kushirikiana nao kujitokeza ili kuunga mkono jitihada hizo kwani ni  jambo  ambalo linakwenda kutengeneza wanamichezo wa baadaye.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa  mradi wa Justfit Foundation, Begam Sykes, amesema dhumuni lao ni kurudisha kile walichokipata kwa jamii ambapo asilimia 10 ya kile kitakachopatikana kupitia mashindano hayo watatumia kukarabati  baadhi ya viwanja.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles