22.6 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 17, 2024

Contact us: [email protected]

Mashabiki Arsenal wamzomea Fabregas

Fabregas-Chelsea-547156LONDON, ENGLAND

KIUNGO wa Chelsea, Cesc Fabregas, alijikuta akiwa na wakati mgumu juzi kwenye Uwanja wa Emirates kutokana na kuzomewa na mashabiki wake wa zamani wa Arsenal.

Nyota huyo wa zamani wa Arsenal ambaye aliitumikia klabu hiyo tangu mwaka 2003 hadi 2011, alionesha kiwango cha hali ya juu akiwa na kikosi chake cha Chelsea na kufanikiwa klabu hiyo kushinda bao 1-0 katika michuano ya Ligi Kuu nchini England.

Hata hivyo, Fabregas alikuwa ni mchezaji bora wa mchezo huo, ila mashabiki hao wa Arsenal walimzomea huku wakidai kwamba ni msaliti wao.

Akizungumza na Sky Sports, Fabregas alidai kwamba kwa sasa amerudi katika ubora wake hivyo atazidi kutoa mchango mkubwa ndani ya klabu hiyo ya darajani.

“Naona kwa sasa nipo katika uwezo wangu, nadhani akili yangu inaweza kufanya maamuzi ya haraka tofauti na miezi michache iliyopita, sijui kwanini lakini nimerudi katika ubora wangu.

“Hali hii yote inatokana na umoja ndani ya klabu nikishirikiana vizuri na wachezaji wenzangu,” alisema Fabregas.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles