20.9 C
Dar es Salaam
Saturday, June 15, 2024

Contact us: [email protected]

Impact yambania Drogba kurudi Chelsea

Didier Drogba,MONTREAL, CANADA

KLABU ya Montreal Impact ya nchini Canada, imesema nyota wa zamani wa Chelsea, Didier Drogba, ataendelea kuitumikia klabu hiyo na kukanusha uvumi kwamba huenda akarejea Stamford Bridge.

Montreal wamesema Drogba ataungana na wachezaji wenzake kwa mazoezi ya kabla kwa ajili ya kuanza kwa maandalizi ya msimu.

Drogba alifanya mazungumzo na Chelsea Desemba mwaka jana kukiwa na uvumi kwamba huenda akarejea katika klabu hiyo msimu huu.

Hata hivyo, Montreal iliweka wazi kwamba nyota huyo wa Ivory Coast ana nia ya kutaka kuisaidia klabu hiyo ya zamani kutokana na matokeo mabaya ambayo wanayapata mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu nchini England.

Kupitia akaunti yake ya Twitter, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 37, aliandika kwamba: “Kwa sasa nipo njiani naelekea Qatar kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu.”

Sasa inaonekana kana kwamba huenda Drogba akatumikia mkataba wake na Montreal ambao unamalizika mwisho wa mwaka huu. Msimu uliopita Drogba ndiye aliyekuwa mfungaji bora wa Montreal, akiwafungia mabao 11. Hata hivyo, mchezaji huyo bado anaonekana kuwa na upendo na klabu hiyo ya zamani ya jijini London.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles