25.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

Giggs kuchukua mikoba ya Van Gaal

Ryan GiggsMANCHESTER, ENGLAND

KOCHA msaidizi wa Klabu ya Manchester United, Ryan Giggs, anaweza kuchukua nafasi ya Van Gaal katika kikosi hicho kutokana na mazungumzo ya uongozi yanavyoendelea.

Van Gaal amekuwa na wakati mgumu ndani ya klabu hiyo kutokana na maendeleo mabaya, hata hivyo wachezaji wenyewe wamekuwa na ushirikiano mdogo na kocha huyo.

Makamu mwenyekiti wa klabu hiyo, Ed Woodward, amefanya mazungumzo na wachezaji wa klabu hiyo juu ya kocha wao hivyo kuna uwezekano mkubwa kocha huyo akafukuzwa.

Kwa mujibu wa mtandao wa The Daily Mail, Woodward ameweka wazi kwamba wachezaji wa klabu hiyo hawana furaha na matokeo na wanakosa ushirikiano na Mholanzi huyo.

Kutokana na hali hiyo, Giggs anaweza kupewa nafasi ya Van Gaal hadi mwishoni mwa msimu huu huku wakihangaika kumtafuta kocha ambaye ataendelea kuitumikia klabu hiyo.

Manchester United ilishuka dimbani mwishoni mwa wiki iliyopita dhidi ya Southampton ambapo ilipokea kichapo cha bao 1-0 kwenye Uwanja wa Old Trafford na kuwafanya mashabiki wa klabu hiyo kumzomea kocha na wachezaji wake.

Kocha huyo alijiunga na klabu hiyo Mei 19 mwaka 2014, kwa mkataba wa miaka mitatu huku akichukua nafasi ya David Moyes, huku Giggs akiteuliwa kuwa kocha msaidizi chini ya Van Gaal.

Hata hivyo, Giggs alihusishwa kuchukua nafasi hiyo wakati United ikiwa inafanya vibaya, huku kukiwa na taarifa kwamba kocha huyo hawezi kudumu ndani ya klabu hiyo kutokana na mwenendo mbaya na nafasi hiyo akitarajiwa kukabidhiwa nyota huyo wa zamani wa United, Giggs.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles