26.3 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 1, 2021

Chameleone: Sijapofuka macho

ChameleoneKAMPALA, UGANDA

NYOTA wa muziki nchini Uganda, Jose Chameleone, amekanusha taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii kwamba anaweza kupofuka macho kutokana na ugonjwa wa ajabu unaomsumbua.

Msanii huyo ameshangaa kuona habari hizo, hata hivyo hajui nani amezisambaza wakati hana tatizo lolote la kiafya.

“Nashukuru kwa wale wote ambao wamekuwa wakinipigia simu mara kwa mara kutaka kujua hali yangu baada ya kusikia nina ugonjwa wa ajabu, ukweli ni kwamba sina ugonjwa wowote, afya yangu ni safi, sielewi nani anasambaza habari hizo.

“Nimechukizwa kwa kuwa simu zimekuwa nyingi zaidi kwa sasa watu wakitaka kujua hali yangu, ila uchunguzi unaendelea kwa ajili ya kumtafuta aliyesambaza habari hizo za uongo mitandaoni,” aliandika Chameleone kwenye akaunti yake ya Twitter.

 

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,628FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles