30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 1, 2023

Contact us: [email protected]

Celine atembelea kaburi la kaka yake

Celine DionNYOTA wa muziki nchini Marekani, Celine Dion, juzi alitembelea kwenye kaburi la kaka yake, Daniel Dion, ambaye alizikwa siku moja baada ya kuzikwa kwa mume wake, Rene Angelil.

Angelil alizikwa Ijumaa ya wiki iliyopita huku kaka yake Celine akizikwa Jumamosi, hivyo Celine alishindwa kuhuzuria mazishi ya kaka yake kwa kuwa familia yake ilimruhusu kuhuzuria mazishi ya mume wake huko huko nchini Canada.

Hata hivyo, juzi msanii huyo aliiomba familia yake impeleke kwenye kaburi la kaka yake alipokwenda kutoa heshima za mwisho.

Kifo cha mume wa Celine na kaka yake vilipishana na kaka wa Celine kwa siku mbili, lakini mazishi yake yalitofautiana siku moja, ndiyo maana Celine alishindwa kuhuzuria mazishi ya kaka yake.

“Nimepoteza watu muhimu katika kipindi hiki, ninaamini siwezi kusahau tukio hilo katika maisha yangu, nitaendelea kuwakumbuka miaka yote kwa kuwa wamekuwa na mchango mkubwa hadi nimefika hapa,” aliandika Celine kwenye akaunti yake ya Twitter.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,396FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles