29.8 C
Dar es Salaam
Sunday, September 15, 2024

Contact us: [email protected]

Depay awaaga rasmi PSV Eindhoven

960EINDHOVEN, UHOLANZI

MSHAMBULIAJI wa Klabu ya Manchester United, Memphis Depay, juzi aliwasili nchini Uholanzi na kuiaga rasmi timu yake ya zamani PSV Eindhoven kwenye Uwanja wa Philips Stadium.

Nyota huyo aliwasili kwenye uwanja huo kwa ajili ya kuiangalia klabu yake ya zamani ikipambana na Twente mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo PSV ilishinda mabao 4-2.

Mchezaji huyo aliwaaga mashabiki wengi ambao walijitokeza uwanjani hapo ambapo walionekana kuwa na furaha kubwa huku wakimpigia makofi.

Mshambuliaji huyo wa Manchester United, hadi sasa amefanikiwa kupachika mabao matano katika michezo 28 aliyocheza tangu alipojiunga katika klabu hiyo kwa kitita cha pauni milioni 25.

Ila bado Manchester United ina wakati mgumu katika msimamo wa ligi huku kwa sasa ikishika nafasi ya tano ikiwa na alama 37 baada ya kucheza michezo 23.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles