24.3 C
Dar es Salaam
Thursday, August 11, 2022

Marekani yajuta kuwaua wanajeshi wa Syria

vitaly-churkin-3DAMASCUS, SYRIA

MAREKANI imesema inasikitika juu ya shambulio lililoongozwa na ndege zake za kivita, ambalo bila kukusudia lililipua kambi za wanajeshi wa Syria.

Makao Makuu ya Jeshi la Marekani yanasema kuwa ndege hizo zilidhani zilikuwa zikishambulia kambi za kundi lijiitalo Dola la Kiislamu (IS), ambazo Marekani ilisema ilikuwa ikizitafuta kwa siku kadhaa.

Lakini Urusi inasema Marekani walikuwa na lengo la kuwasaidia IS na kuongezea kuwa mapatano yake na Marekani kuhusiana na usitishaji wa mapigano yamehatarishwa.

Hakuna habari za kuthibitisha idadi ya watu waliouawa, lakini Urusi ilisema wanajeshi zaidi ya 60 waliuawa, huku wanaharakati wa haki za binadamu wenye makao makuu Uingereza wakitaja idadi ya waliouawa kuwa 80.

Kutokana na hali hiyo Urusi, mshirika mkubwa wa Serikali ya Syria, imetaka ipate maelezo ya kina kutoka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UNSC).

Aidha Balozi wa Urusi kwenye Umoja wa Mataifa (UN), Vitaly Churkin, alitoka nje ya kikao cha dharura cha UNSC kilichokuwa kimeitishwa na taifa hilo kujadili mashambulizi hayo ya Marekani.

Churkin alikuwa akipinga kauli iliyotolewa na Balozi wa Marekani kwenye Umoja huo, Samantha Power, aliyekosoa kile alichokiita ‘unafiki wa Urusi’ na kukifananisha sawa na mazingaombwe.

Marekani ilikuwa imeikosoa Urusi kwa kuitisha mkutano huo maalumu, ikisema hatua hiyo ni kutaka kuwakosoa bila sababu maalumu.

Taarifa ya jeshi la serikali ya Syria pia imelaani mashambulizi hayo, ambayo yamesababisha IS kuingia kirahisi katika maeneo yaliyokuwa yakidhibitiwa na jeshi hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,476FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles