32.2 C
Dar es Salaam
Thursday, February 2, 2023

Contact us: [email protected]

Somalia, Kenya mahakamani zikigombea mpaka

somaliaHAGUE, UHOLANZI

MAOFISA wa Kenya na Somalia kuanzia leo watafika mbele ya Mahakama ya Kimataifa kuhusu Haki (ICJ) kutafuta ufumbuzi wa mgogoro wa mpaka baina yao katika Bahari ya Hindi.

Maamuzi ya mahakama hiyo huenda yakawa na athari kubwa kwa mataifa hayo mawili.

Oktoba 7, 2015, Kenya iliwasilisha hoja ya kupinga hatua ya Somalia kulalamikia mpaka kati ya nchi hizo mbili katika mahakama hiyo yenye makao yake mjini hapa.

Awali Somalia iliwasilisha ombi la kutaka kuchorwa tena kwa mpaka wake na Kenya kwenye Bahari ya Hindi.

Kwa mujibu wa ratiba, Kenya itawasilisha malalamiko yake leo na keshokutwa, huku Somalia ikiwa na nafasi ya kujibu hoja kesho na Ijumaa wiki hii.

“Kuanzia Septemba 19 hadi 23, 2016, ICJ itakuwa ikisikiliza kesi mjini Hague kutathmini hoja iliyowasilishwa na Somalia dhidi ya Kenya, kuhusu mpaka wake na jirani yake ndani ya Bahari ya Hindi,” sehemu ya taarifa iliyotolewa na mahakama hiyo ilisomeka.

Kenya inakataa mahakama hiyo kusikiliza kesi hiyo, ikisema ni kinyume cha mkataba wa mwaka 2009 kati yake na Somalia kuhusu suala hilo.

“Kenya itawakilishwa na Mwanasheria Mkuu Githu Muigai pamoja na ujumbe wa maofisa na kundi la mawakili wa kimataifa,” ilisema ofisi ya mwanasheria mkuu katika taarifa.

Somalia inailalamikia Kenya kwa kujitwalia umiliki wa sehemu ya Bahari ya Hindi, kilomita 100,000 za mraba inayomilikiwa na Somalia.

Kwa sababu hiyo, inaitaka ICJ iuchore upya, baada ya majadiliano juu ya namna ya kuuchora baina ya mataifa hayo kushindikana.

Iwapo hoja ya Somalia ya kugawa mpaka huo itafanikiwa, wachambuzi wa mambo wa Kenya wanadai utaigusa Tanzania, kwani sehemu ya maji yake yatakwenda Kenya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,471FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles