24 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Marekani yaishuku Urusi kukiuka mkataba wa nyuklia

WASHINGTON, Marekani

OFISA wa ngazi ya juu wa intelijensia nchini hapa amesema   huenda Urusi inakiuka mkataba wa nyuklia kwa kufanya majaribio ya silaha zisizo na nguvu kubwa katika ene la Actic.

Akizugumza   mjini hapa jana, Luteni Jenerali Robert Ashley ambaye ni  mkurugenzi wa taasisi ya intelijensia  amesema serikali ya Urusi pengine inakiuka  sheria za mkataba wa  pamoja wa   CTBT unaozuia majaribio ya nyuklia ambao Urusi ilitia saini mwaka 2008  na ambao Marekani imetia saini lakini haijaanza kuutekeleza.

 ”Kwa uelewa wetu uendelezwaji wa silaha za nyuklia unatusababisha tuamini kuwa shughuli za majaribio ya Urusi zitasaidia kuboresha uwezo wa silaha za nyukilia,” alisema Luteni Jenerali Ashley.

Ameongeza kuwa Marekani ilitegemea Urusi, ambayo amesema ilikuwa inategemewa kujaribu silaha zake katika visiwa vya Zemlya  kuongeza ubora wa silaha za nyuklia kwa   muongo mmoja ujao.

Hata hivyo  wachambuzi wa mambo wamepokea taarifa hiyo lakini haikuwashawishi.

 Shirika linalosimamia utekelezaji wa makubaliano ya mkataba wa nyukilia CTBTO, limesema kwenye taarifa yake kuwa haishuku shughuli zozote zinazokwenda kinyume na mkataba.

CTBT unapiga marufuku majaribio ya silaha za nyukilia popote  duniani  uliofikiwa kwenye mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa mwaka 1996.   

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles