24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Mwili wa Tshisekedi wawasili DRC

KINSHASA, DRC

MWILI wa aliyekuwa kiongozi wa upinzani, Etienne Tshisekedi ambaye pia ni baba wa Rais  Felix, ulitarajiwa kuwasili jana baada ya miaka miwili tangu afariki dunia.

Kwa mujibu wa taarifa ya familia, mwili huo utawasili kutoka   Ubelgiji kwa ajili  ya  mazishi.

Kiongozi huyo alifariki dunia mjini Brussels Februari 2017,  akiwa na umri wa miaka 84,  lakini mwili wake ulibaki  katika mji huo mkuu wa Ubelgiji kutokana na wasiwasi wa siasa kwa utawala wa Rais wa zamani wa taifa hili, Joseph Kabila.

Kulingana na taarifa ya nduguye Askofu Gerard Mulumba, mazishi yake yatafanyika katika Viwanja vya Mashahidi.

Askofu Mulumba alisema   baada ya kuukaribisha mwili katika uwanja wa ndege  utasafirishwa hadi katika uwanja huo kwa maombolezo.

Alisema   tayari maandalizi katika uwanja huo ikiwemo ujenzi wa jukwaa umekamilika mbali na yale ya maofisa wa polisi ambao wataongoza gwaride   kumpatia heshima za mwisho baba huyo wa upinzani DRC.

Alisema  takribani marais watano wa bara la Afrika wamethibitisha kuhudhuria mazishi yake.

 ”Ni zaidi ya miaka miwili tangu tulipoanza kutumia kila njia kuusafirisha mwili wake,”  alisema Askofu Mulumba. ”Na sasa kwa kuwa hali iko shwari tunashukuru,” aliongeza.

Akiwa mwanasiasa wa muda mrefu, Tshisekedi alikuwa katika upinzani kwa miongo kadhaa lakini hakufanikiwa kuiongoza nchi hii.

Akiwa mkosoaji mkubwa wa aliyekuwa dikteta Mobutu Sese Seko, alianzisha chama cha Union for Democracy and Special Progress (UDPS) mwaka 1982 baada ya kuachiliwa kutoka jela na mwaka 1997.

Baada ya Mobutu kung’olewa madarakani na kundi lililoongozwa na Laurent Kabila, Tshisekedi alianza kuwa mpinzani wa utawala mpya , msimamo aliokuwa nao hata baada ya mauaji ya Kabila mwaka 2001 huku mwanawe, Joseph akipanda katika hatamu za uongozi.

Baada ya kushindwa katika uchuguzi wa 2011 uliodaiwa kukumbwa na udanganyifu mkubwa , Tshisekedi alikataa kutambua utawala wa Kabila hadi kifo chake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles