27.9 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Raia wa China kizimbani kwa kumtorosha mahabusu polisi

AVELINE KITOMARY -DAR ES SALAAM

RAIA wa China, Cheng Yun Chang (51), amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni, Dar es Salaam, akikabiliwa na shtaka la kumtorosha mtuhumiwa kituo cha polisi.

Wakili wa Serikali, Benson Mwaitenda, aliiambia mahakama kuwa Machi 21, eneo la Kiluvya katika Kituo cha Polisi Gogoni, Wilaya ya Ubungo, mshtakiwa alimtorosha Cheng Yang ambaye ni mtoto wake aliyetuhumiwa kuiba nyaya za umeme zenye thamani ya Sh milioni 8.

Mshtakiwa alikanusha kutenda kosa hilo, Wakili Mwaitenda alisema upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na kuomba tarehe ya kutajwa tena.

Wakili wa mshtakiwa, Deogras Mari, aliiomba mahakama kumpatia mteja wake dhamana kutokana na kosa hilo kudhaminika kisheria.

Hakimu Godfrey Isaya alisema dhamana iko wazi kwa mshtakiwa kwa kupeleka hati ya kusafiria na kuwa na mdhamini mmoja anayefanya kazi serikalini.

Hata hivyo mshtakiwa alishindwa kukidhi masharti ya dhamana na kurudishwa rumande hadi kesi yake itakaposomwa tena Juni 3.

Wakati huo huo, wanafunzi watatu wamepandishwa kizimbani kwa shtaka la kukutwa na dawa za kulevya aina ya bangi.

Waliopandishwa kizimbani ni Jackson Munisi (21), Salum Ramadhan (20) na Omary Amir (18) ambao ni wanafunzi.

Akisoma shtaka hilo mbele ya Hakimu Boniface Lihamwike, Wakili wa Serikali, Veronika Mtafia alidai Machi 21 eneo la Mabibo Kanuni, Wilaya ya Kinondoni, washtakiwa walikutwa na bangi yenye uzito wa kilo 46.34.

Wote walikana kutenda kosa hilo huku upande wa Jamhuri ulisema upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na kuomba tarehe ya kutajwa tena.

Washtakiwa walishindwa kukidhi masharti ya dhamana na kurudishwa rumande hadi kesi yake itakaposomwa tena Juni 6, mwaka huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles