21.2 C
Dar es Salaam
Saturday, August 13, 2022

Mapigano ya wakulima, wafugaji yanapogeukia kwa viongozi

Jamii na Afya concept.inddNa MOHAMED HAMAD – MANYARA
WILAYA ya Kiteto iliyopo mkoani Manyara, imekuwa na migogoro ya ardhikati ya wakulima na wafugaji hali iliyosababisha watu kushindwakufanya shughuli zingine za maendeleo na wengine kujeruhiwa na hatakuuawa.

Kufuatia migogoro hiyo, baadhi ya idara mbalimbali za Serikali kamaafya,maji na elimu zilionekana kusuasua kutokana na migogoro hiyohali liyosababisha manung’uniko makubwa kwa wananchi juu ya Serikaliyao.

Hali hiyo ilidaiwa kuwacheleweshea wananchi maendeleo kwa miakaminne mfululizo, wasijue cha kufanya huku baadhi yao wakipoteza maisha
na wengine kujeruhiwa wakati wakigombea ardhi, jambo lililosukumaSerikali kuunda tume mbalimbali kuichunguza.

Mbali na kupoteza maisha wengi walipata ulemavu wa kudumu, na umaskinikwa kuteketezewa mali zao zikiwemo pikipiki, mazao na kuwafanyawaishi kwa taabu katika maisha yao, hali iliyolazimu baadhi yawatumishi wa Serikali kuhamishwa vituo vya kazi.

Waliohamishwa ni pamoja na baadhi ya wakuu wa idara, watendaji wavijiji  na hata wanasiasa kushindwa kurejea katika nyazifa zao wakatiwa uchaguzi, kufuatia madai kuwa wamechangia migogoro hiyo.

Kwa miaka miwili, Wilaya ya Kiteto ilidaiwa kuwa shwari haliiliyosababisha wananchi wengi kuanza kurejea katika hali zao zakawaida kwa kufanya shughuli za kilimo na wengine ufugaji kwalengo la kujipatia kipato cha kuendesha maisha yao.

Utulivu huo ulisababishwa na tume kadhaa zilizoundwa na aliyekuwaWaziri Mkuu, Mizengo Pinda, kutaka kujua kiini chamigogoro hiyo na kuitafutia ufumbuzi ambapo waliweza kufanya kazi kwazaidi ya siku 60.

Baadhi ya viongozi walieleza chanzo cha migogoro ya ardhiKiteto kuwa ni kukosekana kwa uadilifu kwa baadhi ya viongozi wa vijijiambao wametajwa kuuza ardhi kinyemela kinyume cha Sheria ya ArdhiNamba 5 ya Mwaka 1999.

VIONGOZI

Akizungumza na wenyeviti wa vijiji 68 pamoja na watendaji wao,Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara, Eliakimu Maswi, anasema Serikaliimebaini chanzo cha migogoro na kuwataka watumishi kujipima kamawanaendana na kasi ya Rais Magufuli na ikiwezekana waache kazi kabla yakutumbuliwa.

“Tumebaini kuwa wenyeviti wa vijiji na watendaji wao wamekuwa vinarawa kuuza ardhi, sasa hatuna nafasi ya kuwabembeleza, tutawatumbua nakuwafikisha mahakamani…hatutamwonea haya mwenyekiti tutawakamata.
“Uwezo wa kijiji kutoa ardhi ni ekari 50, zaidi ya hapo ni
wilaya na kiwango cha juu zaidi ni Wizara. Inakuwaje mwenyekiti wakijiji au kitongoji atoe zaidi ya ekari 1,000, 2,000 na hata 5,000…mamlaka hayo anapata wapi?

“Mkuu wa Wilaya naomba sasa tufanye kazi na wala usisitekumchukulia hatua mwenyekiti wa kijiji, muweke ndani haraka unapoonakuwa amefanya makosa kwa makusudi, kwa kufanya hivyo tutapunguzauhalifu huu,”anasema Maswi.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Tumain Magessa,nasema alilazimika kuita kikao cha kazi na viongozi wa vijijiili kuanza ukurasa upya wa kuwavusha salama wanachi wa Kitetowaweze kufanya kazi bila ubughudhiwa.

MAPIGANO YA KARIBUNI

Wakati kukiwa na mikakati hiyo, wiki iliyopita Diwani wa Kata ya Kaloleni, wilayaniKiteto mkoani humo, Christopher Parmet (CCM), alinusurika kifobaada ya kuchomwa mkuki na watu wanaodaiwa kuwa ni wafugaji wakatiwakiswaga mifugo iliyokuwa imeingia shambani kwake.

Tukio hilo lilitokea maeneo ya Kisima Kata ya Amei, wilayani Kitetowakati diwani huyo na wafanyakazi wake, Chibundiki Naisoni (54) naHarold Mtalima (56) wakiswaga mifugo iliyokuwa imeingia shambani na
kula mazao aina ya mbaazi.

“Baada ya kupigiwa simu na wafanyakazi wangu wa shambani kuwang’ombe wameingia shambani, niliamua kwenda na kuwakuta. Tulimpigia simu mwenye mifugo ili aje lakini alikataa akisisitizamifugo yake iachiwe mara moja,” anasema.

Diwani huyo anasema kufuatia hali hiyo aliamuru ipelekwe kwa uongozi waKitongoji na wakati wakiiswaga, ghafta lilijitokeza kundi la vijana
wa kimasai na kuanza kurusha fimbo na mikuki ambapo waliwezakumchoma mkuki mkono wa kulia na wasaidizi wake kujeruhiwa sehemumbalimbali za miili yao.

Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Tumaini Magessa, anasemaalipigiwa simu na diwani huyo aliyekuwa akidai anaishiwa nguvu baadaya kuvuja damu nyingi kwa kuchomwa mkuki na kuagiza Polisi kwenda
kumchukua.

Anasema matukio hayo awali yalikoma lakini inaonekana kufanywa nawafugaji wa wilaya za jirani na kutoweka ambapo amedai jitihada zakukabiliana na tukio hilo ni kuwa na daftari la wakazi kila kijiji ili
kuwabaini wahalifu.

Mbunge wa Jimbo la Kiteto, Emmanuel Papian (CCM), anazitaka mamlaka zaSerikali kama Mahakama na Polisi  kutimiza wajibu wao ili kukomeshamatukio hayo ambayo aliyaita kuwa ni ya kujirudia kwa utochukuliwahatua madhubuti.

Anasema matukio hayo ni mwendelezo wa mauaji yaliyokwisha fanyikaKiteto.

Ambapo anasema wilaya imejipanga kukabiliana na tukio hilo la kihalifuakisisitiza kuwa kila mamlaka zitimize wajibu wao sambamba na wananchikutoa taarifa mapema kukabiliana na matukio hayo ya kikatili.

Mwenyekiti wa wenyeviti 68 Wilayani Kiteto, Salimu Mbwegu, akizungumzakwenye kikao maalumu kilichoitwa ‘Mwanzo mpya wa kuirejesha Kiteto
yenye amani’, chini ya Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, anasema njia pekee ya kukabiliana na migogoro ni kila mmoja kutimizawajibu wake.

“Baadhi ya wenyeviti na watendaji wao wanalalamikiwa kuhusika katikamigogoro ya ardhi, lakini hivi wenyeviti wanalipwa?

“Kwaninihawalipwi, wanafanyaje kazi za erikali…tunaitaka Serikali kuwalipapamoja na kutoa asilimia 20 za vijiji ili waweze kujiendesha,” anasema Mbwegu.

Akijibu hoja hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa  ßalmashauri ya Wilaya yaKiteto, Tamimu Kambona, anawahakikishia wenyeviti hao kuwawameandaliwa malipo yao sambamba na asilimia 20 za vijiji japo si zote iliwapate cha kuanzia katika maendeleleo ya vijiji.

Kambona pia anawaonya baadhi ya watumishi wa Serikali ambao niwaleviwa kupindukia kuwa hatowavumilia na kwamba sheria kali zitachukuliwa dhidi yao,sambamba na kuwafukuza akidai utawala huu ni wa tofauti.

USHAURI

 

Asasi zinazofanya kazi na wafugaji wa asili nchini zinashauriSerikali kwa kushirikiana na wadau iwe na mkakati wa pamoja wa kuelimisha umma juu ya umuhimu wa amanibaina ya makundi yote katika jamii na kulinda haki ya kila mmoja.

Serikali kwa kushirikisha wadau ifanye mapitio juu ya sera na sheria zinazogusa masilahi ya wafugaji na wakulima ili kubaini maeneo yanayohitaji maboresho katika utekelezaji kwa ajili ya ukuaji wa mfumo mzima wa uzalishaji mali, ustawi wa amani na mshikamano miongoni mwa makundi yote ya jamii.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,590FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles